• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, October 8, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Zitto Kabwe: Mahakama ya Rufani imethibitisha CAG Mstaafu Prof.Mussa Assad aliondolewa kinyume cha Katiba

Asema Mahakama haikuamuru arejeshwe katika nafasi yake wala alipwe fidia

by bajeti
October 7, 2026
in Habari
0
Zitto Kabwe: Mahakama ya Rufani imethibitisha CAG Mstaafu Prof.Mussa Assad  aliondolewa kinyume cha Katiba

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu (CAG) Prof.Mussa Assad

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

KIONGOZI Mstaafu wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe amesema  Mahakama ya Rufani imethibitisha kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu (CAG) Prof.Mussa Assad kuondolewa kwake kulikuwa kinyume cha Katiba,

Hata hivyo Mahakama haikuamuru arejeshwe katika nafasi yake wala alipwe fidia.

Zitto ameeleza kuwa Mahakama ya Rufani ilithibitisha kuwa kifungu cha 6(1) cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma, kilichoweka kipindi cha miaka mitano cha kushika nafasi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kinachoweza kuongezwa mara moja, ni kinyume cha Katiba.

Kiongozi Mstaafu wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe

Kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo ameyasema hayo leo Oktoba 7,2026 katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kufuatia Hukumu ya Mahakama ya Rufani Juu ya Kuondolewa Kinyume cha Katiba kwa Profesa Mussa Assad katika nafasi ya CAG iliyotolewa Oktoba 6, 2026.

Zitto amesema Mahakama ilithibitisha kuwa kuondolewa kwa Profesa Mussa Assad tarehe 3 Novemba 2019, kwa madai kwamba kipindi chake kilikuwa kimeisha, kulikuwa kinyume cha Katiba.

“Mahakama ilitupilia mbali rufaa kinzani ya Serikali iliyopinga maamuzi hayo,pia ilitupilia mbali rufaa yetu iliyotaka nafuu zaidi, ikiwemo kurejeshwa kwa Profesa Assad katika nafasi yake.

“Hukumu hii inathibitisha kuwa muda wa CAG kushika madaraka unaongozwa na Katiba na  Ibara ya 144 (1) inalipa Bunge mamlaka ya kuweka umri wa kustaafu, lakini hailipi mamlaka ya kuweka kipindi maalumu cha kushika madaraka”amesema Zitto

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu (CAG) Prof.Mussa Assad

Aidha amesema kuwa kuondolewa kabla ya kustaafu kunaruhusiwa tu kwa sababu zilizoainishwa katika Katiba na kwa kufuata ushauri wa baraza maalum lililoundwa kwa mujibu wa Katiba.

“Mahakama pia ilikataa hoja kwamba kuondolewa kwa Profesa Assad kungeweza kuhalalishwa kwa sababu, wakati huo, sheria iliyotumika ilikuwa bado haijatangazwa kuwa kinyume cha Katiba.

“Ilieleza kuwa kufanya hivyo kungehalalisha kuingiliwa kinyume cha Katiba kwa muda wa kushika madaraka wa mwenye wadhifa wa kikatiba.

“Huu ndio ulinzi tuliokwenda mahakamani kuutetea”amebainisha Zitto

Hata hivyo Zitto amefafanuwa kuwa CAG anakagua fedha za umma kwa niaba ya wananchi,na uhakika wa kuendelea kushika madaraka kwa mujibu wa Katiba unamwezesha kufanya kazi kwa uhuru, bila hofu ya kuondolewa na Serikali.

“Rais hawezi kumwondoa CAG kihalali kwa sababu tu kipindi cha miaka mitano kimeisha.

 “Hata hivyo, nimesikitishwa na uamuzi wa Mahakama wa kutotoa nafuu yenye kuleta suluhisho kwa Profesa Assad kutokana na kuondolewa kwake kinyume cha Katiba.

“Mahakama ilikataa kumrejesha kazini kwa sababu iliona kwamba aliyemrithi aliteuliwa kihalali chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma, na kwamba kumrejesha kungesababisha watu wawili kushika nafasi moja.”ameongeza Zitto

Zitto amebainisha kuwa Mahakama pia ilikataa kutoa fidia, ikieleza kuwa hili lilikuwa shauri la kikatiba kuhusu wadhifa wa umma, badala ya mgogoro wa kawaida wa ajira.

“Hakuna amri iliyotolewa kuhusu gharama za shauri,naiheshimu Mahakama, lakini sikubaliani na uamuzi wake kuhusu nafuu.

“Kwa mtazamo wangu, kuitetea Katiba kunapaswa pia kujumuisha kurekebisha madhara yanayotokana na ukiukwaji wake,Prof. Assad aliondolewa kabla ya kufikia umri halali wa kustaafu.

“Lakini, licha ya kuthibitisha kuwa kuondolewa kwake kulikuwa kinyume cha Katiba, Mahakama haikuamuru arejeshwe katika nafasi yake wala alipwe fidia.”amebainisha Zitto

Zitto ameelezea pia kuwa hukumu hiyo inawalinda watakaoshika nafasi hiyo baadaye, lakini haijatoa suluhisho kwa madhara aliyopata Profesa Assad.

“Hilo bado ni jambo linalotia wasiwasi mkubwa, Mawakili wangu wataendelea kuchukua hatua stahiki kukamilisha hili.

“ Hata hivyo, msimamo wa kikatiba uko wazi: kipindi cha miaka mitano kinachoweza kuongezwa mara moja, kilichowekwa na kifungu cha 6(1), kilikuwa kinyume cha Katiba.

“Kuondolewa kwa Profesa Assad kwa msingi huo pia kulikuwa kinyume cha Katiba na maamuzi haya yanaimarisha uhuru wa CAG na uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma na tulikwenda mahakamani kuitetea Katiba na katika masuala hayo ya msingi, Mahakama ya Rufani imekubaliana na msimamo wetu”amesema Zitto

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:0
  • Today's page views 0
  • Total visitors 22,403
  • Total page views 24,964

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In