• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, October 15, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Kakoso:Tunahitaji wawekezaji lakini wanahitajika kufuata sheria

by bajeti
October 15, 2026
in Mazingira
0
Kakoso:Tunahitaji wawekezaji lakini wanahitajika kufuata sheria

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Miundombinu Selemani Kakoso (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji 1-01 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali mbele ya Kamati za Kudumu za Bunge ikiwemo ya Maji na Mazingira pamoja na ya Miundombinu katika kikao cha akiwasilisha maoni ya Serikali kuhusu maombi ya Chama cha BOPOA - Lake Zone kufanya mapitio ya kifungu cha 57 (1) cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira na kanuni zake ili kuruhusu matumizi maalumu ya Ukanda wa Mita 60 kwa shughuli za Kibandari kama ilivyoelekezwa na Tangazo la Serikali (GN) Namba 293 la Mwaka 2022, kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Bunge jijini Dodoma leo Oktoba 15, 2026. 2 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Miundombinu Mhe. Selemani Kakoso (kulia) na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Jackson Kiswaga wakiwa katika kikao cha kuwasilisha maoni ya Serikali kuhusu maombi ya Chama cha BOPOA - Lake Zone kufanya mapitio ya kifungu cha 57 (1) cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira na kanuni zake ili kuruhusu matumizi maalumu ya Ukanda wa Mita 60 kwa shughuli za Kibandari kama ilivyoelekezwa na Tangazo la Serikali (GN) Namba 293 la Mwaka 2022, kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Bunge jijini Dodoma Oktoba 15, 2026.

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,DODOMA

MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Miundombinu  Selemani Kakoso amesema wanahitaji uwekezaji ili kuifanya nchi isonge mbele lakini wawekezaji wanahitajika kufuata sheria.

Kakoso ameyasema hayo baada ya kusikiliza maoni ya Serikali kuhusu maombi ya Chama cha BOPOA – Lake Zone kufanya mapitio ya kifungu cha 57 (1) cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira na kanuni zake ili kuruhusu matumizi maalumu ya Ukanda wa Mita 60 kwa shughuli za kibandari kama ilivyoelekezwa na Tangazo la Serikali (GN) Namba 293 la Mwaka 2022.

Kakoso amesema ni muhimu kwa wadau kushiriki katika vikao vya kutoa maoni kuhusu mabadiliko ya sheria mbalimbali vinavyoitishwa na Bunge ili mchango wao uweze kufanyiwa kazi.

Kakoso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanganyika ameongeza kuwa ni kweli wanahitaji uwekezaji ili kuifanya nchi isonge mbele lakini wawekezaji wanahitajika kufuata sheria.

“Mazingira yameharibiwa hivyo wana wajibu wa kuyasimamia ili yarudi katika hali yake“amesema Kakoso

Kakoso ameelekeza wawekezaji BOPOA – Lake Zone kufanya shughuli zao kwa kufuata miongozo na sheria ya mazingira na kufanya kazi kwa ukaribu na NEMC kwakuwa wao ndio wanaosimamia mazingira kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais.

Baadhi ya wabunge na wataalamu wakiwa katika kikao cha kuwasilisha maoni ya Serikali kuhusu maombi ya Chama cha BOPOA – Lake Zone kufanya mapitio ya kifungu cha 57 (1) cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira na kanuni zake ili kuruhusu matumizi maalumu ya Ukanda wa Mita 60 kwa shughuli za Kibandari kama ilivyoelekezwa na Tangazo la Serikali (GN) Namba 293 la Mwaka 2022, kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Bunge jijini Dodoma leo Oktoba 15, 2026.

Akizungumza mbele ya Kamati hiyo,Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Reuben Kwagilwa  amesema Serikali haitakuwa kikwazo kwa wawekezaji wenye nia ya kufanya uwekezaji wa miradi ya maendeleo bali itaendelea kuwawekea mazingira wezeshi na kusimamia sheria ili mazingira yasiharibiwe.

Kwagilwa amesema Serikali itaendelea kusimamia na kuhakikisha kuwa shughuli za kibandari nchini zinafanyika kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa, huku ikiimarisha ushirikiano kati ya taasisi za umma na sekta binafsi.

Amesisitiza kuwa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) halipo kwa ajili ya kuzuia miradi bali inafanya kazi yake kuhakikisha wadau wanatimiza wajibu wao kwa kufanya shughuli zao kwa kufuata sheria bila kuchafua mazingira.

Aidha,Kwagilwa amebainisha kuwa kwa kutambua umuhimu wa bandari katika kuchochea ukuaji wa uchumi na kuongeza pato la taifa, Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kuendeleza miundombinu ya bandari na kuboresha uendeshaji wa shughuli za kibandari nchini.

“Mheshimiwa Mwenyekiti lengo la kufanya haya yote ni kuongeza ufanisi, kuvutia uwekezaji na kuimarisha mchango wa sekta ya usafiri wa majini katika maendeleo ya nchi,“ amesema Kwagilwa.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Reuben Kwagilwa akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali mbele ya Kamati za Kudumu za Bunge ikiwemo ya Maji na Mazingira pamoja na ya Miundombinu katika kikao cha akiwasilisha maoni ya Serikali kuhusu maombi ya Chama cha BOPOA – Lake Zone kufanya mapitio ya kifungu cha 57 (1) cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira na kanuni zake ili kuruhusu matumizi maalumu ya Ukanda wa Mita 60 kwa shughuli za Kibandari kama ilivyoelekezwa na Tangazo la Serikali (GN) Namba 293 la Mwaka 2022, kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Bunge jijini Dodoma Oktoba 15, 2026.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Jackson Kiswaga, Naibu Waziri wa Uchuzi David Kihenzile, Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Maduhu Kazi pamoja na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), NEMC na Chama cha BOPOA-Lake Zone.

Next Post
Mhandisi Masauni:Tanzania imeweka utaratibu wa kisheria kugawa mapato ya biashara ya Kaboni

Mhandisi Masauni:Tanzania imeweka utaratibu wa kisheria kugawa mapato ya biashara ya Kaboni

Makamu wa Rais Ndejembi:Tanzania kuuza umeme nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Makamu wa Rais Ndejembi:Tanzania kuuza umeme nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:40
  • Today's page views 42
  • Total visitors 22,546
  • Total page views 25,124

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In