• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Sunday, October 18, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Dkt.Muyungi:Agenda ya nishati safi ya kupikia ni mojawapo ya nyenzo za kupunguza ukataji wa miti

by bajeti
October 17, 2026
in Mazingira
0
Dkt.Muyungi:Agenda ya nishati safi ya kupikia ni mojawapo ya nyenzo za kupunguza ukataji wa miti

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi (wa kwanza kushoto) akiwa na viongozi mbalimbali mara baada ya kuchangia Majadiliano ya Kibunge kuhusu Hali ya Hewa na Uhifadhi wa Asili yaliyofanyika katika Jiji la Yerevan nchini Armenia Oktoba 13 hadi 15, 2026.

Share on FacebookShare on Twitter

YEREVAN,ARMENIA

KATIBU Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi anesena agenda ya nishati safi ya kupikia ni mojawapo ya nyenzo za kupunguza ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa.

Amesema usimamizi shirikishi wa misitu iliyopo katika vijiji kwa jamii yenyewe inayoizunguka imesaidia katika kukuza na kuendeleza biashara ya kaboni na kuleta faida nchini Tanzania.

Dkt. Muyungi ameyasema hayo Oktoba 15,2026 wakati akichangia Majadiliano ya Kibunge kuhusu Hali ya Hewa na Uhifadhi wa Asili yaliyofanyika katika Jiji la Yerevan nchini Armenia.

Amesema Tanzania inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, agenda ya nishati safi ya kupikia ni mojawapo ya nyenzo za kupunguza ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa.

Dkt. Muyungi amesema misitu iliyopo nchini inaweza kupotea endapo ukataji wa miti utaendelea hivyo matumizi ya nishati safi ya kupikia itasaidia kuhifadhi bioanuwai na kupunguza ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa.

 “Misitu iliyopo nchini ipo hatarini kupotea endapo ukataji wa miti utaendelea hivyo agenda ya matumizi ya nishati safi ya kupikia itasaidia kuhifadhi bioanuwai na kupunguza ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa.

“Kwa hatua hiyo sisi kama Tanzania tumeshaivuka lengo la asilimia 30 ifikapo mwaka 2030, kati ya hekta milioni 48.1 za ardhi ya Tanzania tumeshahifadhi zaidi ya asilimia 33, hiyo ni kupitia hifadhi za taifa, mapori ya akiba, eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, pamoja na maeneo mengi ya vijiji ambayo yameshahifadhiwa”amesema Dkt.Muyungi

Aidha,Dkt.Muyungi  ameeleza kuwa dhamira na maono ya Tanzania kwa miaka 25 ijayo imezindua Dira ya Maendeleo 2050 ambayo inasema “tunahitaji kuwa na uchumi wa Dola Trilioni 1 ifikapo mwaka 2050, matarajio ya kuishi miaka 75 na kipato cha mtu mmoja mmoja cha Dola 7,000.”

“Hatua hii ina maana kubwa kwa namna Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais inavyosimamia matamanio hayo pamoja na uhifadhi wa mazingira na bioanuwai hasa katika nguzo ya Ustahimilivu wa Mazingira”ameongeza Dkt.Muyungi  Katika hatua nyingine Dkt.Muyungi amebainisha kuwa kuwa Tanzania ina hekta zaidi ya milioni 2 za ardhi ya vijiji ambavyo vinajihusisha na biashara ya kaboni akitolea mfano misitu aina ya mikoko (mangrove) akieleza kuwa ina thamani kubwa zaidi.

“Msitu wa mikoko ndio wenye thamani kubwa zaidi kwani hekta moja inaweza kuhifadhi takribani tani 1,000 za hewa ya ukaa kwa mwaka, hii imeongeza thamani ya mikoko na kuongeza hamasa zaidi kwa jamii kushiriki katika biashara ya kaboni na kujipatia kipato,” amesema Dkt. Muyungi

Kikao hicho cha majadiliano kilifanyika kando ya Mkutano wa 17 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Bioanuai (CBD COP17) kuanzia Oktoba 13 hadi 15, 2026 na kilishirikisha wabunge kutoka Armenia kwa lengo la kuleta manufaa yanayoonekana katika nyanja mbalimbali ili kudumisha uhifadhi.

Next Post
Kakonko ‘wamkuna’Waziri Masauni matumizi ya nishati safi ya kupikia, ujenzi kiwanda cha kuzalisha tani 730 za mkaa mbadala

Kakonko ‘wamkuna’Waziri Masauni matumizi ya nishati safi ya kupikia, ujenzi kiwanda cha kuzalisha tani 730 za mkaa mbadala

Askofu Gwajima: aliyewapeleka waumini wetu mahabusu wametoka na hawaogopi mabomu ya machozi

Askofu Gwajima: aliyewapeleka waumini wetu mahabusu wametoka na hawaogopi mabomu ya machozi

Joseph Kabila,Rais Mstaafu wa Kongo, uliyewafanyia mema wakongo,shukrani yao ni kumhukumu kifo,na kumfilisi mali zake

Joseph Kabila,Rais Mstaafu wa Kongo, uliyewafanyia mema wakongo,shukrani yao ni kumhukumu kifo,na kumfilisi mali zake

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:2
  • Today's page views 2
  • Total visitors 22,590
  • Total page views 25,184

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In