• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Friday, May 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Spika Dkt.Tulia aieleza IPU juhudi za serikali katika kudumisha amani

by bajeti
March 13, 2023
in Habari
0
Spika Dkt.Tulia aieleza IPU juhudi za serikali katika kudumisha amani

Spika wa Bunge Dkt.Tulia Ackson ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kundi la Afrika katika Umoja wa Mabunge Duniani akihutubia Mkutano Mkuu wa 146 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaoendelea nchini Bahrain juu ya juhudi za Serikali ya Tanzania katika kudumisha amani na mahusiano mazuri ya kijamii kwa wananchi Machi 12,2023.Picha na Bunge

Share on FacebookShare on Twitter

MANAMA,BAHRAIN

SPIKA wa Bunge Dkt. Tulia Ackson amehutubia Mkutano Mkuu wa 146 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaoendelea nchini Bahrain na kueleza  juhudi za Serikali ya Tanzania katika kudumisha amani na mahusiano mazuri ya kijamii kwa wananchi.

Spika Dkt.Tulia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kundi la Afrika katika Umoja wa Mabunge Duniani (Africa Geopolitical Group in the IPU),ameyasema hayo Machi 12,2023 wakati akihutubia mkutano huo wenye kauli mbiu “Kukuza Amani na Kujenga Jamii Jumuishi yenye Kuvumiliana”.

Dkt. Tulia amezungumzia kuhusu juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Bunge katika kudumisha amani na mahusiano mazuri ya kijamii kwa wananchi wake pamoja na kuheshimu Maazimio ya Kimataifa katika kulinda na kudumisha amani Duniani.

Wakati huohuo, Dkt. Tulia amewasilisha hoja ya dharura ya kuundwa kwa Mfuko wa Maafa Duniani kwa ajili ya kusaidia Nchi zinazoathiriwa na majanga ya asili na mabadiliko ya tabianchi.

Pamoja na hoja hiyo, hoja zingine nne zilizowasilishwa na Mataifa mengine  zinatarajiwa kupigiwa kura ya maamuzi ili Umoja huo upitishe hoja moja ya dharura ambayo itajadiliwa, kuboreshwa na hatimaye kutengeneza azimio la Mkutano huo.

 

 

 

Next Post
Kamati ya Bunge

Kamati ya Bunge

Dkt.Mpango awapa Wakuu wa Wilaya mbinu za Uongozi Bora

Dkt.Mpango awapa Wakuu wa Wilaya mbinu za Uongozi Bora

Bilioni 4.2 zatumika kuendeleza bunifu za Sayansi na Teknolojia

Bilioni 4.2 zatumika kuendeleza bunifu za Sayansi na Teknolojia

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:0
  • Today's page views 0
  • Total visitors 16,333
  • Total page views 18,523

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In