• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Bilioni 4.2 zatumika kuendeleza bunifu za Sayansi na Teknolojia

by bajeti
March 17, 2023
in Habari
0
Bilioni 4.2 zatumika kuendeleza bunifu za Sayansi na Teknolojia

Waandishi wa habari wakiangalia gari lililofungwa kiti cha kuruhusu watu wenye ulemavu wa miguu kuliendesha kwa kutumia mikono kilichobuniwa na Mhandisi Joseph Taifa jijini Dar es Salaam Machi 8,2023 baada ya kuendelezwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).Picha na Goodluck Hongo

Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO

TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imetumia zaidi ya Sh.Bilioni 4.2 ili kuendeleza ubunifu uliofanywa na watafiti wa kitanzania katika kuhakikisha kuwa  unawanufaisha watanzania kwa kubadilisha maisha yao.

Mbali na hilo lakini pia Tume hiyo chini ya Mkurugenzi  wake Dkt. Amos Nungu imefanikiwa kuwatambua wabunifu 2647 katika kipindi cha kuanzia mwaka 2018 hadi 2022.

Takwimu hizo zimetolewa Machi 8,2023 jijini Dar es Salaam na Mwakilishi wa Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Kuendeleza Sayansi,Teknolojia na Ubunifu(MTUSATE) Dickson Mjarifu wakati wa Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kati ya waandishi wa habari na watafiti yaliyoandaliwa na COSTECH.

Amesema wabunifu 283 wamepatiwa msaada wa kitaalamu kutoka katika taasisi mbalimbali za kiserikali ili kuendeleza bunifu zao kwa manufaa ya nchi na watanzan ia wote

“kuanzia mwaka 2018 hadi 2022 COSTECH tumewatambua wabunifu 2647 katika ya hao 283 wamepatiwa msaada wa kitaalamu na 178 wamepatiwa fedha ili kuendeleza bunifu zao na ”amesema Mjarifu

Mjarifu ameongeza katika kipindi hicho pekee kiasi cha Sh.Bilioni 4.26 zimetumika kwa wabunifu 178 ili waweze kuendeleza vitu walivyobuni kwa manufaa ya kuwanufaisha wananchi.

Hata hivyo Mjarifu amebainisha baadhi ya wabunifu waliofaidika na COSTECH ni pamoja na mtanzania aliyebuni Majipesa ambapo mtu nawezan kuweka hela kujipatia maji kulingana na kiwango cha fedha alizoweka.MAXCOM Afrika na nyingine nyingi ikiwemo mita za maji ambazo unalipia kabla ya matumizi.

Kwa upande wake Mratibu wa Mafunzo hayo kutoka COSTECH Deusdeth Leonaed amebainisha kuwa hayo ni mafunzo ya tisa tangu yalipoanzishwa mwaka 2015 na kufanyika katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Unguja,Pemba,Dodoma,Mwanza na Arusha.

Next Post
Majaliwa:Wananchi lindeni vyanzo vya maji na mazingira

Majaliwa:Wananchi lindeni vyanzo vya maji na mazingira

Wenye ulemavu wa miguu sasa kuendesha magari

Wenye ulemavu wa miguu sasa kuendesha magari

Jafo:Wakuu wa wilaya wekeni mikakati kupunguza matumizi ya mkaa,kulinda ukataji miti

Jafo:Wakuu wa wilaya wekeni mikakati kupunguza matumizi ya mkaa,kulinda ukataji miti

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In