• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Dkt.Mpango awapa Wakuu wa Wilaya mbinu za Uongozi Bora

by bajeti
March 17, 2023
in Habari
0
Dkt.Mpango awapa Wakuu wa Wilaya mbinu za Uongozi Bora

Makamu wa Rais wa Dkt. Philip Mpango akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Angellah Kairuki, waliokaa (Kushoto),Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama (kulia),Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Daniel Chongolo (wa kwanza kushoto)na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Wilaya wanaoshiriki mafunzo ya uongozi mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo jijini Dodoma Machi 13,2023.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,DODOMA

MAKAMU wa Rais Dkt. Philip Mpango amewataka Wakuu wa Wilaya nchini kuzingatia utawala bora,kanuni na sheria ikiwemo kudhibiti uvujaji wa siri za serikali kwa kujiepusha na matumizi yasiofaa ya mitandao ya kijamii na barua pepe binafsi katika kutuma nyaraka za serikali.

Mbali na hilo lakini pia amewataka kuzingatia utaratibu katika matumizi ya walinzi binafsi na waandishi wa habari katika ofisi za umma  pamoja na  utatuzi wa migogoro katika maeneo yao.

Dkt.Mpango ameyasema hayo Machi 13, 2023 wakati akifungua Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Wilaya yanayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jiji la Dodoma uliopo Mtumba.

Amesema ni vema viongozi hao kuzingatia maadili ikiwemo kwa kujiepusha na matumizi yasiofaa ya mitandao ya kijamii na barua pepe binafsi katika kutuma nyaraka za serikali.

Amesema ni muhimu kwa viongozi hao kuwa wepesi na wabunifu katika kutatua migogoro hususani migogoro ya ardhi na mipaka, migogoro baina ya wakulima na wafugaji na baina ya wafugaji au wakulima na hifadhi na kuhakikisha hakuna migogoro mipya inayoibuka katika maeneo yao.

Ameongeza kuwa viongozi hao wana wajibu wa kudhibiti uhasama ndani ya jamii au na vyombo vya dola, mauaji na kuwa walinzi wa haki za watu wote hususani wanawake na watoto.

Hata hivyo Dkt.Mpango amewataka   kusimamia miradi inayotekelezwa katika maeneo yao  kwa kuhakikisha inakamilika kwa wakati na viwango vilivyokusudiwa na kuongeza jitihada katika ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri, kudhibiti matumizi yasiyo na tija pamoja na kuziba mianya yote inayosababisha fedha nyingi za Serikali kupotea na  kuhakikisha malipo mbalimbali katika maeneo yao yanafanyika kielektroniki na fedha zinapelekwa benki kwa wakati.

Aidha amefafanua kuwa viongozi hao wanatakiwa kuwa walinzi maadili, mila , desturi na utamaduni wa mtanzania kwa kutofumbia  macho mmomonyoko wa maadili wa aina yeyote utakaojitokeza katika maeneo wanayosimamia.

“Mjiepusha na rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka pamoja na kutenda haki kwa wananchi na watumishi walio chini yao kuwahudumia  wananchi kwa staha, kusikiliza kero na kuzitafutia ufumbuzi kwa wakati na  kuwa makini wakati wote mnapozungumza na Umma kwa kuhakikisha mnatumia lugha fasaha na nzuri.

“Ni lazima pia kuimarisha utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwa kutoa hamasa kwa wananchi hususani vijana ili wawe mstari wa mbele katika shughuli za uhifadhi ikiwemo kupanda miti na kusimamia mipango miji katika maeneo yao.”amesema Dkt.Mpango

Dkt Mpango ameongeza kuwa pamoja na masuala mengine lakini pia wasimamia suala la uhifadhi wa vyanzo vya maji na matumizi ya nishati mbadala ili kupunguza utegemezi mkubwa wa kuni na mkaa.

Kwa Upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaan (OR-TAMISEMI) Angellah Kairuki amesema Wizara hiyo imelenga kuongeza jitihada katika usimamizi wa miradi ya maendeleo, kuongeza jitihada katika ukusanyaji wa mapato na udhibiti wa matumizi, kuweka mkazo katika uwezeshaji wa wananchi kiuchumi, uendelezaji miji pamoja na kuhamasisha maendeleo vijijini.

Aidha amewataka Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanawahudumia vema wawekezaji na wenye nia ya kuwekeza hapa nchini kwa kuwa wafuatiliaji na kuondoa vikwazo kwenye masuala ya uwekezaji katika maeneo wanayosimamia.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama amewaasa Wakuu wa Wilaya kuhakikisha huduma bora zinawafikia wananchi, kutenda haki kwa watumishi wote na kuwa na mshikamano ikiwemo kusimamia medani za siasa na utawala bora na kuwachukulia hatua watumishi wote wanaoenda kinyume na kanuni, sheria na miongozo ya utumishi wa umma.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amesema ni muhimu kwa viongozi hao  kusimamia kikamilifu suala la migogoro ya ardhi,wakulima na wafugaji ambayo inasababishwa na viongozi katika maeneo husika kutotimiza wajibu wao kikamilifu.

 

Next Post
Bilioni 4.2 zatumika kuendeleza bunifu za Sayansi na Teknolojia

Bilioni 4.2 zatumika kuendeleza bunifu za Sayansi na Teknolojia

Majaliwa:Wananchi lindeni vyanzo vya maji na mazingira

Majaliwa:Wananchi lindeni vyanzo vya maji na mazingira

Wenye ulemavu wa miguu sasa kuendesha magari

Wenye ulemavu wa miguu sasa kuendesha magari

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In