• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Sunday, May 3, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Maafisa Ardhi watakiwa kutoa elimu kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji

by bajeti
October 7, 2023
in Mazingira
0
Maafisa Ardhi watakiwa kutoa elimu kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji

Mkuu wa Wilaya ya Mvovmero Mkoa wa Morogoro Judith Nguli akizungumza Oktoba 6,2023 wakati wa uzinduzi wa Kampeni Maalumu ya ‘Tutunzane Mvomero‘ yenye lengo la kuepusha migogoro baina ya wakulima na wafugaji wilayani Mvomero mkoani Morogoro.Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Khamis Hamza Khamis na Kulia ni Naibu Waziri wa Mifugo Alexander Mnyeti (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,MOROGORO

NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Khamis Hamza Khamis amewataka Maafisa Ardhi nchini kutoa elimu ya matumizi bora ya ardhi ili ili kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji.

Khamis ametoa agizo hilo Oktoba 6,2023 wilayani Mvomero Mkoa wa Morogoro wakati wa uzinduzi wa Kampeni Maalumu ya ‘Tutunzane Mvomero‘ yenye lengo la kuepusha migogoro ya makundi hayo mawili.

Mbali na hilo lakini pia amewataka wananchi kutunza mazingira kwa kuepuka kukata miti hovyo pamoja na ufugaji usio wa kisasa unaosababisha uharibifu wa mazingira.

Amesema migogoro ya wakulima na wafugaji inasababisha uharibifu mkubwa ukiwemo wa mazao, mifugo kuuliwa na kuacha majeraha na vifo kwa binadamu.

“Tupunguze migogoro ya wakulima na wafugaji, hebu twendeni tukawafundishe watu wetu namna bora ya kusimamia matumizi ya ardhi ninaamini kila wilaya ina maafisa ardhi, na hili ni agizo la Serikali,“ amesema Khamis.

Hata hivyo kutokana na changamoto ya ukataji miti kiholela na sekta za mazingira, nishati na ardhi ni mtambuka,Khamis  ametoa wito kwa maafisa hao kutoa elimu kwa wananchi kuhusu nishati safi ya kupikia.

“Miti inakatwa sana mimi nimetokea Dar es Salaam nimepita barabarani hasa maeneo ya Morogoro na Pwani unapishana na pikipiki zimepakia mkaa, kama mtakumbuka Rais wetu alifungua mjadala wa nishati safi ya kupikia, maana yake anataka tufanye transormation ya nishati tutoke kwemye kuni na mkaa twende kwenye mishati nyingine ya gesi au umeme,“ amesisitiza Khamis.

Katika hatua nyingine,Khamis  amesisitiza wananchi kuendelea kupanda miti ikiwa ni maelekezo ya Serikali na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi kuwa kila Halmashauri kupanda miti milioni 1.5 kila mwaka ili kuifanya nchi kuwa ya kijani.

Next Post
Sita wavuliwa uanachama CHADEMA

Sita wavuliwa uanachama CHADEMA

Spika Dkt.Tulia aomba kura mkutano wa  147 wa IPU nchini Angola

Spika Dkt.Tulia aomba kura mkutano wa 147 wa IPU nchini Angola

Tanzania kuwa mwanachama wa GGGI

Tanzania kuwa mwanachama wa GGGI

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:9
  • Today's page views 10
  • Total visitors 16,045
  • Total page views 18,204

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In