• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Tanzania kuwa mwanachama wa GGGI

Kufaidika na uwekezaji miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

by bajeti
October 27, 2023
in Mazingira
0
Tanzania kuwa mwanachama wa GGGI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Global Green Growth (GGGI) Dkt. Frank Rijsberman (kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini Mhe. Togolani Mavura (wa tatu kushoto), Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria Ofisi ya Makamu wa Rais Dustan Shimbo (wa pili kulia) na watendaji wengine wa Serikali mara baada ya kikao baina ya viongozi hao wawili kilichofanyika Oktoba 26,2023 jijini Seoul,Korea Kusini (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU.KOREA KUSINI

 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Global Green Growth (GGGI) Dkt. Frank Rijsberman jijini Seoul nchini Korea Kusini.

Taasisi hiyo ya kimataifa yenye makao makuu yake katika Jiji la Seoul nchini Korea Kusini, ina takriban wanachama 48 na kati yao sita wanatoka katika Bara la Afrika Afrika.

Katika mazungumzo ambayo yamefanyika Oktioba 26,2023 nchini humo pamoja na mambo mengine  wamejadiliana pia kuhusu utayari wa nchi kuwa mwanachama wa GGGI na kushirikiana na taasisi hiyo kuijengea uwezo Tanzania katika kuandaa programu, miradi na mikakati ya kufaidika na fedha na uwekezaji wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi (climate financing).

Aidha, Waziri Dkt. Jafo ameshiriki Mkutano Mkuu wa 12 na Kikao cha 16 cha Baraza la Nchi Wanachama wa Taasisi ya Kimataifa ya GGGI wenye kujadili masuala mbalimbali kuhusu uhifadhi ya mazingira.

Taasisi hiyo ya kimataifa yenye makao makuu yake katika Jiji la Seoul nchini Korea Kusini, ina takriban wanachama 48 na kati yao sita wanatoka katika Bara la Afrika Afrika.

Katika hatua nyingine akiwa katika ziara hiyo ya kikazi, Waziri Mhe. Dkt. Jafo amepata nafasi ya kushiriki katika mkutano na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Korea Kusini.

Mjadala katika mkutano huo ni kuhusu ni  fursa zilizopo katika nchi hiyo za mazingira ambazo Tanzania inaweza kunufaika nazo zikiwemo Biashara ya Kaboni (Carbon Credit), Uchumi wa Buluu (Blue Economy) na Udhibiti wa Taka (Waste Management).

Waziri Jafo yupo ziarani nchini Korea Kusini kwa ziara ya kikazi ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuimarisha ushirikiano katika masuala ya mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Next Post
Njombe-Tanzania

Njombe-Tanzania

Uhusiano wa Tanzania na India waimarika

Uhusiano wa Tanzania na India waimarika

Wajukuu wawili wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wafariki kwa ajali ya gari 

Wajukuu wawili wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wafariki kwa ajali ya gari 

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:6
  • Today's page views 6
  • Total visitors 13,062
  • Total page views 14,807

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In