• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Wajukuu wawili wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wafariki kwa ajali ya gari 

by bajeti
November 15, 2023
in Habari
0
Wajukuu wawili wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wafariki kwa ajali ya gari 

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Butiama Jumanne Sagini akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Edward Magige ambaye ni Mjukuu wa Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere wakati wa Ibada kuuaga mwili wake iliyofanyia katika Kanisa Katoliki Parokia ya Butiama mkoani Mara Novemba 14, 2023.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,BUTIAMA

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini na Mbunge wa Jimbo la Butiama ameshiriki Ibada ya mazishi ya marehemu Edward Magige ambaye ni Mjukuu wa Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere, iliyofanyika kijijini kwao wilayani Butiama Mkoa wa Mara.

Marehemu Magige alifariki Novemba 11, 2023 kwa ajali iliyotokea huko mkoani Shinyanga,ambapo pia alikuwa mtumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ambacho ni moja kati ya chombo kilichopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi hadi umauti ulipomfika.

Huo unakuwa msiba wa pili ndani ya mwezi mmoja tangu kutokea kwa msiba wa kwanza wa marehemu Daudi Charles Makongoro ambaye ni mjukuu wa Baba wa Taifa na mtoto wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere aliyefariki Oktoba 29, 2023 kwa ajali ya gari iliyotokea katika barabara ya bypass Jijini Arusha.

Akizungumza katika mazishi hayo Novemba 14, 2023, Naibu Waziri Sagini ametoa pole kwa familia, Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Wafanyakazi wa NIDA Mkoa wa Shinyanga, ndugu, jamaa na marafiki na kuwaomba wazidi kumuombea marehemu aendelee kupumzika kwa amani.

 “Baada ya kupata taarifa ya ajali pia nikaarifiwa kuwa alikuwa ni mtumishi wa NIDA huko mkoani Shinyanga na mimi kama Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi pia natoa pole kwa Mkurugenzi Mkuu na Watumishi wote,” amesema Sagini.

Aidha Viongozi mbalimbali wa Kiserikali, Kidini na Kisiasa walishiriki mazishi hayo akiwamo Mkuu wa Wilaya ya Butiama Moses Kaegele, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mara Julius Masubo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama ambaye pia ni baba mdogo wa marehemu Peter Wanzagi na Chifu wa Kabila la Wazanaki Japhet Wanzagi

Next Post
Mahakama yasimama kwa muda kuhakiki kitambulisho cha mwandishi

Kesi ya Lydia Lugaga dhidi ya Damas Ndumbaro kutolewa hukumu Novemba 23,2023

Rais Samia atoa bilioni 1.4 kujenga ofisi ya RPC Mara

Rais Samia atoa bilioni 1.4 kujenga ofisi ya RPC Mara

Mvua tishio Dar es salaam

Mvua tishio Dar es salaam

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In