• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Kesi ya Lydia Lugaga dhidi ya Damas Ndumbaro kutolewa hukumu Novemba 23,2023

by bajeti
November 16, 2023
in Habari
0
Mahakama yasimama kwa muda kuhakiki kitambulisho cha mwandishi
Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

MAHAKAMA Kuu Divisheni ya Ardhi inatarajiwa kutoa hukumu kesi ya Rufaa namba 253/2022 inayomhusu Lydia Paulo Lugaga dhidi ya Damas Daniel  Ndumbaro baada ya pande zote kukamilisha taratibu zilizohitajika.

Kesi hiyo ya mgogoro wa ardhi iliyo chini ya Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu Division  ya Ardhi  Crecensia Kisongo inatarajiwa kutolewa hukumu mnamo Novemba 23,2023 baada ya kusikiliza kwa njia ya maandishi.

Uamuzi wa kusikilizwa shauri hilo kwa njia ya maandishi ulifikiwa Septemba 11,2023 baada ya wakili wa Damas Ndumbaro,Neema Masawe kuiomba Mahakama hiyo kusikiliza shauri hilo kwa njia ya maandishi.

Wakili upande wa mlalamikaji Pasensa Dickson amesema Oktoba 17,2023 waliitwa ili kuendelea na shauri hilo ambapo upande unaolalamikiwa ulishakamilisha utaratibu wote kama unavyohitajika katika kesi zinazosikilizwa kwa njia ya maandishi baada ya wao nao kukamilisha.

“Sasa tunasubiri maamuzi ya mahakama baada ya kujiridhisha kwa pande zote mbili kutekeleza utaratibu wa kimahakama kama ulivyohitajika”amesema Dickson

Septemba 11,2023,Mahakama hiyo iliamuru mwadishi wa habari wa Bajeti Communication Goodluck Hongo kupelekwa mbele ya Ofisi ya Afisa Utumishi wa Mahakama hiyo ili iweze kuhakiki kitambulisho chake (press card) baada ya kutaka kuripoti kesi ya Rufaa namba 253/2022 inayomhusu Lydia Paulo Lugaga dhidi ya Damas Daniel  Ndumbaro.

Uamuzi huo ulikuja wakati rufaa hiyo ilipoanza kusikilizwa muda mfupi baada ya Karani wa Mahakama kuwaita wahusika wa shauri hilo kwa kutumia kipaza sauti kama ilivyo utaratibu wa kila siku wa kuitwa kwa mashauri mbalimbali katika mahakama hiyo.

Mara baada ya kuingia katika chumba cha mahakama ,Wakili anayemtetea Damas Ndumbaro, Neema Masawe aliieleza  Mahakama hiyo kuwa kuna mtu aliyeingia ndani ya Mahakama hiyo ajitambulishe yeye ni nani ili afahamike kabla ya kesi kuendelea.

Hata hivyo Hongo alijitambulisha mbele ya Naibu Msajili wa Mahakama hiyo Kisongo kuwa yeye ni mwanahabari na yupo hapo kusikiliza na kuripoti shauri hilo,

Lakini  Masawe aliiambia Mahakama hiyo  kuwa kesi hiyo inamhusu Mheshimiwa Waziri hivyo haitakiwi kuripotiwa na vyombo vya habari.

“Mheshimiwa kesi hii inamhusu mheshimiwa Waziri hivyo haitakiwi kuripotiwa na vyombo vya habari,lakini hata hivyo ipo “Chamber court”amesema Masawe

Mara baada ya kauli hiyo,Naibu Msajili Mfawidhi Kisongo alipitia kitambulisho cha mwandishi huyo na kisha kumwelekeza Karani wa Mahakama kuongozana naye hadi kwa Afisa Utumishi ili aweze kukihakiki.

“Peleka kwa Afisa Utumishi aweze kuhakiki hiki kitambulisho nawe mfuate huko”amesema Naibu Msajili Mfawidhi Kisongo

Hata hivyo Ofisi ya Afisa Utumishi ilikuwa imefungwa na badala yake Karani huyo alielekea katika Ofisi nyingine ya Afisa Utumishi ambayo ilikuwa na watu na baada ya kuonesha press card hiyo alishauriwa kumwambia  mwandishi huyo kuwa atoke nje na kisha kuwasubiri mawakili wa pande zote ndipo awahoji.

“Umeambiwa utoke nje kule chini na uwasubiri mawakili wote wakishatoka ndio uwahoji, nimeambiwa hivyo nikwambie”amesema Karani wa Mahakama hiyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana.

 

Next Post
Rais Samia atoa bilioni 1.4 kujenga ofisi ya RPC Mara

Rais Samia atoa bilioni 1.4 kujenga ofisi ya RPC Mara

Mvua tishio Dar es salaam

Mvua tishio Dar es salaam

Dkt.Jafo:Bonde la  Ziwa Tanganyika ni nyumbani kwa watu zaidi ya milioni 13

Dkt.Jafo:Bonde la Ziwa Tanganyika ni nyumbani kwa watu zaidi ya milioni 13

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:6
  • Today's page views 6
  • Total visitors 13,062
  • Total page views 14,807

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In