• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Dkt.Jafo:Bonde la Ziwa Tanganyika ni nyumbani kwa watu zaidi ya milioni 13

Asema ni zaidi ya kapu la chakula

by bajeti
November 18, 2023
in Mazingira
0
Dkt.Jafo:Bonde la  Ziwa Tanganyika ni nyumbani kwa watu zaidi ya milioni 13

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo (wa pili kushoto)akishuhudia makabidhiano ya uenyekiti wa Mkutano wa Mawaziri waliopo katika Mkataba wa Kikanda wa Usimamizi Endelevu wa Ukanda wa Ziwa Tanganyika (LTA) kutoka kwa Mwenyekiti anayemaliza muda wake Mhandisi Prosper Dodiko (kushoto) ambaye ni Waziri wa Mazingira, Kilimo na Mifugo wa Burundi kwa Mhandisi Dkt. Collins Nzovu ambaye ni Waziri wa Uchumi wa Kijani na Mazingira wa Zambia wakati wa Mkutano wa 11 wa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Ziwa Tanganyika uliofanyika jijini Lusaka, Zambia Novemba 17, 2023.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI MAALUM,ZAMBIA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)  Dkt. Selemani Jafo  amesema Ziwa Tanganyika ni zaidi ya kapu la chakula na nyumbani kwa watu zaidi ya milioni 13  hivyo ni lazima kulinda,kuhifadhi mazingira na rasilimali zake ili liendelee kuinufaisha jamii na kuleta maendeleo endelevu.

Amesema ni wajibu wetu kuhakikisha changamoto zinazolikabili zikiwemo kupungua kwa kina cha maji, uchafuzi wa mazingira kutoka viwandani na majumbani, upotevu wa bayoanuai na mchanga zinakwisha.

Dkt. Jafo ametoa wito Novemba 17,2023 jijini Lusaka nchini Zambia wakati akifungua Mkutano wa 11 wa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Ziwa Tanganyika uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mulungushi

Dkt. Jafo amesema ziwa hilo ni urithi wa shughuli za kiuchumi na kijamii zinazofanywa ndani ya bonde zikiwemo uvuvi, kilimo, ufugaji, makazi ya watu na uchimbaji madini.

“Tutambue kuwa Ziwa Tanganyika ni zaidi ya kapu la chakula kwa jamii zetu na bonde lake ni nyumbani kwa zaidi ya watu milioni 13, ni eneo bora kwa kuunganisha nchi zetu nne zinazolizunguka, hivyo hatuna budi kushirikiana kwa pamoja katika uhifadhi na matumizi sawa ya rasilimali zake,” amesema Dkt.Jafo

Aidha, Dkt. Jafo amesema kuwa mkutano huo ni muhimu katika kutathmini hatua iliyofikiwa kuelekea matumizi endelevu ya rasilimali na utekelezaji wa miradi chini ya mpango wa kikanda, hii ni fursa ya kutoa mwongozo kuelekea lengo hilo. Mkutano pia umetumika tukio la kutia saini Itifaki ya Maendeleo ya Ufugaji wa Majini katika Ziwa Tanganyika na bonde lake.

Hata hivyo amewashukuru wadau wa maendeleo kwa juhudi zao katika usimamizi endelevu wa Ziwa Tanganyika kupitia miradi wanayotekeleza na kusema kuwa Serikali ya Tanzania inalichukulia kwa uzito mkubwa suala la maendeleo endelevu ya Bonde la Ziwa Tanganyika.  Akifunga mkutano huo Dkt. Jafo amempongeza Waziri wa Uchumi wa Kijani na Mazingira wa Serikali ya Zambia Mhe. Mhandisi Dkt. Collins Nzovu kwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Baraza Kuu la Mawaziri.

Katika mkutano huo, washiriki wamepokea na kujadili masuala mbalimbali muhimu yakiwemo taarifa za uchambuzi wa uwezekano wa kuwajumuisha Makatibu Wakuu katika Vyombo vya Sheria vya LTA, Itifaki ya Maendeleo ya Kilimo cha Majini kwa Ziwa Tanganyika na bonde lake;.

Taarifa zingine ni utafiti kuhusu maeneo muhimu ya bioanuwai katika Ziwa Tanganyika na bonde lake, hali ya utekelezaji wa miradi mbalimbali, hali ya michango ya kitaifa na mpango wa kazi wa mwaka na bajeti ya LTA ya mwaka 2024.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wa Mkutano wa 11 wa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Ziwa Tanganyika uliofanyika jijini Lusaka, Zambia Novemba 17, 2023. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Mkutano huo umehudhuriwa pia na Waziri wa Mazingira, Kilimo na Mifugo wa Burundi ambaye ni mwenyekiti anayemaliza muda wake Mhandisi Prosper Dodiko, Waziri wa Uvuvi na mifugo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Adrien Bokele Djema na Mkurugenzi Mtendaji wa LTA Sylvain Tusanga Mukanga.

Ujumbe ulioshiriki katika Mkutano huo uliwashirikisha pia Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira)  Abdallah Hassan Mitawi, Mkurugenzi wa Mazingira Kemilembe Mutasa na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Dkt. Deogratius Paul.

Baraza hilo linaundwa na mawaziri kutoka nchi nne ambazo ni Tanzania, Zambia, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Next Post
Mashauriano kuhusu wakandarasi wazawa

Mashauriano kuhusu wakandarasi wazawa

UNEP kuendelea kufadhili miradi ya mazingira Tanzania

UNEP kuendelea kufadhili miradi ya mazingira Tanzania

Israel imeshindwa kuwapata mateka wake zaidi ya 200 waliotekwa na Hamas

Israel imeshindwa kuwapata mateka wake zaidi ya 200 waliotekwa na Hamas

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In