GAZA,PALESTINA
KWA mara ya kwanza katika historia ya Dunia,Taifa la Israel lililokuwa likijulikana kama Taifa la Mungu kutokana na kuandikwa na kutabiriwa katika vitabu vya Dini hasa ya Kikristo limeshindwa vita dhidi ya Kundi la wapiganaji la Hamas kutoka Ukanda wa Gaza-Palestina.
Kushindwa huko kunakuja baada ya mapigano ya siku zaidi ya 40 tangu Israel ilipoanzisha mashambulizi ya kulipiza kisasi baada ya shambulio la Hamas ndani ya ardhi za Israel mnamo Oktoba 7,2023 licha ya Jeshi la Israel kulizingira eneo hilo kwa miaka zaidi ya 10.
Tangu kutokea kwa shambulio hilo viongozi mbalimbali wa nchi za Ulaya akiwemo Rais wa Marekani,Joe Biden walizuru Taifa la Israel ili kuliunga mkono kutokana na kitendo cha Hamas, kundi linalodaiwa kuungwa mkono na Iran ambalo linadaiwa kuwaua zaidi ya waisrael 1000 na wengine zaidi ya 200 kuwateka nyara.
Licha ya Israel kuwa na vikosi vya kisasa vyenye uwezo mkubwa katika vita,teknolojia na vifaa kikiwemo kikosi chake maarufu kama MOSSAD limeshindwa kuwapata mateka zaidi ya 200 waliotekwa katika uvamizi wa ajabu uliofanya na kundi la Hamas mnano Oktoba 7,2023 ndani ya ardhi za Israel.
Hata hivyo Israel ikisaidiwa na Nchi za Ulaya pamoja na Marekani ambayo ilipeleka manowari za kubebea ndege vita katika eneo la ukanda huo kuisaidia Israel inayoaminika kuwa na vikosi vyenye uwezo wa hali ya juu na kuingia Ukanda wa Gaza imeambulia patupu kuwapata mateka wao wakiwemo wanajeshi jambo linaloibua maswali mengi.
Kitendo cha Jeshi la Israel cha kushindwa kuwapata na kuwakomboa mateka hao,kimeonesha kuwa Jeshi la Israel na washirika wake limeshindwa vita hivyo kwa kundi dogo lisilokuwa na vifaru,vifaa vya kisasa vya kijeshi zaidi ya kutumia silaha za kawaida katika kukabiliana na Jeshi la kisasa la Israel na washirika wake Marekani.
Mbali na hilo lakini pia Israel kukubali kusitisha vita kwa siku nne na kundi la Hamas ikiwemo kubadilishana wafungwa 150 wa kipalestina dhidi ya 50 wa Israel ni wazi kuwa MOSSAD haiwezi tena kukabiliana na kundi hilo hivyo Israel inapaswa kuwa makini kwa siku zijazo la sivyo itapigwa katika hatua za kushangaza hadi katika Mji Mkuu wake wa Jerusalem au Tel Aviv.
Israel pia imeshindwa kuliangamiza kundi hilo kama inavyoelezwa kutokana na kwamba licha ya Israel kufanya mashambulizi makali lakini viongozi wa Hamas wanaendelea na mikutano na viongozi wengi nje ya nchi,hivyo ni wazi kuwa haitaweszekana kuliangamiza kundi hilo ambalo nchi za Magharibi zinalitambua kama kundi la kigaidi lakini Urusi,Uturuki,Iran na baadhi ya nchi za kiarabu linawatambua kama wapigania uhuru wa Taifa la Palestina
Vita hivyo badala ya kuwaadhibu wanamgambo hao wa Hamas,vimewafanya wananchi wa Gaza-Palestina kutolewa kafara ambapo hadi sasa zaidi ya wapalestina 14,000 na zaidi ya 1000 raia wa Israel wameuawa




Discussion about this post