• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Friday, May 29, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

‘Mapapa’ wa dawa za kulevya sasa yatumia drone,mitandao ya kijamii

by bajeti
July 27, 2024
in Habari
0
Tani dawa za kulevya ‘zautikisa’ mwaka 2023.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kuthibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania Aretas Lyimo

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

‘MAPAPA’ wanaojishughulisha na biashara za dawa za kulevya sasa wameingia katika matumizi ya teknolojia ya hali ya juu ikiwemo kutumia ndege isiyo na rubani (drone) katika kufanikisha lengo lao.

Mbali na kutumia teknolojia hiyo lakini pia wafanyabishara hao wameamua kutumia mitandao  ya siri na fedha za kidijitali.

Kitendo cha kutumia teknolojia ya kisasa katika kufanya biashara hiyo,kunaonesha kuwa mapambanano dhidi ya mapapa hao sio jambo jepesi na ni la hatari zaidi kwa maisha ya binadamu.

Hayo yamebainishwa katika  Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya ya Mwaka 2023 nchini Tanzania iliyotolewa Mwezi Mei,2024 na kusainiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,(Sera,Bunge na Uratibu) Jenista Mahagama na Kamishna Jenerali Mamlaka ya Kuthibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) Aretas Lyimo na kueleza kuwa katika kipindi cha mwaka 2023 mafanikio makubwa yaliyopatikana yalitokana na uwezeshaji mkubwa wa Serikali pamoja na utashi wa kisiasa katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana zipo changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa majukumu ya kupambana na dawa za kulevya nchini.

Baadhi ya changamoto zilizotajwa katika taarifa hiyo ya mwaka 2023 juu ya kukabili uthibiti wa mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini ni pamoja na mabadiliko ya teknolojia.

‘’Mabadiliko ya teknolojia inayotumika katika biashara ya dawa za kulevya ikihusisha matumizi ya mitandao ya mitandao ya kijamii,vifaa vya kisasa kama ndege isiyokuwa na rubani ,mitandao ya siri na fedha za kidijitali.

”Taarifa hiyo imebainisha kuwa watumiaji wa intaneti duniani ni asilimia 66 ya watu wote na asilimia 59 kati yao hutumia mitandao ya kijamii ambapo miongoni mwa faida za teknolojia ni kurahisisha upatikanaji wa huduma za tiba ya uraibu kwa kutumia simu na mawasiliano mengine ya kimtandao

‘’Matumizi mabaya ya teknolojia huathiri faida za teknolojia na kurudisha nyuma maendeleo,kwa mfano Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya  ya Dunia ya mwaka 2023 ilionesha ongezeko kubwa la uuzaji wa dawa za kulevya kwa njia ya mitandao ya siri(Dark Web) na zaidi ya robo tatu ya wanaume wanaotumia dawa za kulevya walinunua kupitia mitandao ya siri”amefafanua taarifa hiyo

Taarifa hiyo imenukuu Utafiti uliofanyika mwaka 2021 nchini Ireland,ulionesha kuwa asilimia 64 ya mauzo ya dawa za kulevya yalifanyika kupitia mitandao ya kijamii,asilimia 28 kupitia mitandao ya siri(Dark Web) na asilimia nane kupitia maduka ya mtandaoni(Online shop)

‘’Kwa mwaka 2022,asilimia 0.2 ya miamala iliyofanywa kwa njia ya fedha za kidijitali (Crypocurrencies)ilikuwa kwa ajili ya kuuza na kununua dawa za kulevya’’imeongeza taarifa hiyo.

Hata hivyo kutokana na nguvu na uwezo kifedha walionao,aliyekuwa Rais wa Ufilipino Rodrigo Durtete aliendesha kampeni yikiwemo kuwapiga risasi watu wote wanaojihusisha na biashara hiyo baada ya kuona kizazi cha Taifa hilo kinaangamia hali iliyozusha malalamiko juu ya haki za binadamu

 

 

Next Post
Makamu wa Rais Dkt Mpango asafiri kwa Treni ya SGR

Makamu wa Rais Dkt Mpango asafiri kwa Treni ya SGR

Jeshi la Polisi Tanzania laonya watumiaji mitandao ya kijamii

Jeshi la Polisi Tanzania laonya watumiaji mitandao ya kijamii

NHC kubadili eneo la Urafiki kuwa kitovu cha maendeleo ya kiuchumi

NHC kubadili eneo la Urafiki kuwa kitovu cha maendeleo ya kiuchumi

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:10
  • Today's page views 10
  • Total visitors 16,603
  • Total page views 18,841

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In