• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Monday, May 4, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

TFRA:Matumizi ya mbolea yafikia tani 840,000 mwaka 2023/2024

Yawatunuku vyeti vijana 192 baada ya kufuzu mafunzo ya biashara ya mbolea

by bajeti
September 23, 2024
in Mazingira
0
TFRA:Matumizi ya mbolea yafikia tani 840,000 mwaka 2023/2024

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent akizungumza na vijana zaidi ya 100 (hawapo pichani) waliofuzu mafunzo ya uendeshaji wa biashara ya mbolea wa Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (Building a Better Tomorrow - BBT) Septemba 22,2024 wilayani Chamwino Mkoa wa Dodoma.(Picha na mpigapicha wetu)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,DODOMA

MKURUGENZI  Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent amesema matumizi ya mbolea nchini yameongezeka kutoka tani 500,000 kwa mwaka 2022/2023 hadi kufikia tani 840,000 mwaka 2023/2024 .

Ongezeko hilo limetokana ya ruzuku ya Mbolea inayotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Laurent ametoa kauli hiyo Septemba 22,2024 Chinangali ll wilayani Chamwino Mkoa wa Dodoma, wakati akikabidhi vyeti vya mafunzo ya uendeshaji wa biashara ya mbolea kwa vijana 192 wa Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (Building a Better Tomorrow – BBT)

Amesema ongezeko la matumizi ya mbolea nchini ni kubwa hadi kufikia tani 840,00 na hiyo inaashiria kwamba  jamii imeelimika kuhusu matumizi ya mbolea.

“Ongezeko la matumizi ya mbolea ni kubwa,na hii inaashiria namna jamii ilivyoelimika na kutambua umuhimu wa mbolea kwenye shughuli zao za kilimo,

‘’TFRA inaendelea kupanua wigo wa utoaji elimu juu ya matumizi sahihi ya mbolea kwa wakulima ili waendelee kunufaika” amebainisha Laurent 

Baadhi ya Vijana waliofuzu mafunzo ya uendeshaji wa biashara ya mbolea wa Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (Building a Better Tomorrow – BBT) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent hayupo (pichani) kabla ya kutunukiwa vyeti na Mamlaka hiyo wilayani Chamwino Mkoa wa Dodoma Septemba 22,2024.(Picha na mpigapicha wetu)

Akizungumzia vijana 192 waliotunukiwa vyeti na Mamlaka hiyo,Laurent ameeleza kuwa kwa kutambua umuhimu wa miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Wizara ya Kilimo, TFRA imeratibu mafunzo hayo kwa kushirikiana na Idara ya Mafunzo ya Wizara ya Kilimo kupitia Vyuo vya Mafunzo ya Kilimo (MATI) ili kutoa mafunzo ya uendeshaji wa biashara ya mbolea kwa kuzingatia Sheria ya Mbolea Na. 9 ya mwaka 2009.

Aidha amefafanuwa kuwa vyeti hivyo vitawasaidia vijana hao kujisajili kuwa mawakala wa pembejeo za mbolea.

‘’Ninawapongeza vijana wa BBT kutokana na mafunzo mliyopata,ambayo yatawajenga katika Kilimo mnachoendelea kufanya.

‘’Mafunzo ya siku mbili yaliyotolewa kwenu yana maana kubwa katika maandalizi ya msimu wa kilimo unaoelekea kuanza hivi karibuni”ameongeza Laurent

Hata hivyo Laurent ameishukuru Wizara ya Kilimo kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuwalea vizuri vijana wa BBT jambo linalochangia kuzidi kukua kwa Sekta ya Kilimo nchini.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa Jenga Kesho Iliyobora (BBT) Mathed Kahaya ameishukuru TFRA kwa mafunzo waliyotoa na kuongeza kuwa mafunzo hayo yawe endelevu na yasiishie hapo kwani yatasaidia kuwakumbusha vijana hao mambo ya kuzingatia kwenye Kilimo chao mara kwa mara.

Next Post
Upendo kwa watoto

Upendo kwa watoto

ACT-Wazalendo yaeleza mikakati yake kudhibiti biashara dawa za kulevya

ACT-Wazalendo yaeleza mikakati yake kudhibiti biashara dawa za kulevya

Upendo kwa Wazee

Upendo kwa Wazee

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:0
  • Today's page views 0
  • Total visitors 16,049
  • Total page views 18,208

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In