NA MWANDISHI WETU
CHAMA Cha Sauti ya Umma (SAU) kimesema kitadhibiti wanaharakati wenye nia ovu na wanaofadhiliwa na watu wasio wema endapo kitapata mamlaka ya kushika dola kwa kuwapa wagombea wake kura nyingi za ndio katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Mbali na hilo lakini pia katika wiki 40 baada ya kuingia madarakani, SAU itafufua na kukamilisha mchakato wa kupata katiba mpya uliokwamishwa na baadhi ya vyama vya siasa mwaka 2014.
SAU kimebainisha kuwa italinda uhuru wa kitaifa na kupinga kuingiliwa na mataifa ya kigeni endapo kitapata ridhaa ya wananchi kukichagua kuongoza Serikali.
Kwa mujibu wa Ilani ya Chama hicho yenya kauli mbinu Amani,Uadilifu na Maendeleo iliyopitishwa April 28,2025 ni Ilani yenye nguzo muhimu za Kilimo, Viwanda na Teknolojia inaeleza kuwa ni ya ukombozi kwa mtanzania ambapo juu ya nguzo hizo SAU inakwenda kuboresha maisha ya watanzania na maendeleo ya taifa.
“Ilani hii ni mtiririko wa ahadi za chama kwa wapiga kura na watanzania wote, inaonyesha dira, maadili, sera na mipango ya chama katika kipindi cha miaka mitano ya utawala na kwa jinsi gani tutaweza”imefafanuwa Ilani hiyo
Hata hivyo kwa upande wa masuala ya Ulinzi,Ilani ya SAU imebaisnisha kuwa Serikali yake itaendelea kuimarisha ulinzi wa mipaka yetu na kudhibiti wanaharakati wenye nia ovu na wanaofadhiliwa na watu wasio wema.
“Kuzingatia sheria, uwazi na uwajibikaji,kuendelea kuimarisha ulinzi wa miaka yetu na kudhibiti wanaharakati wenye na ovu na wanaofadhiliwa na watu wasio wema.
“Kuboresha sheria na kutumia nguvu kazi za wahalifu hususani wadogo wadogo kuzalisha pato la taifa badala ya kufungiwa na kula, kulala bure
“Kuanzisha idara maalamu ya upelelezi inayojitegemee na kushirikiana na vyombo vya dola kukomesha usafirishaji, ulimaji na utumiaji madawa ya kulevya”imebainisha Ilani hiyo
Hata hivyo Serikali ya SAU itafanya maboresho ya sheria na kutoa ruzuku kwa vyama vyote vya siasa ili kutengeneza usawa na haki katika malezi ya vyama na demokrasian ikiwemo kupambana na rushwa
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho Betha Mpata amesema Ilani imefafanua ni jinsi gani chama cha sauti ya umma kitakavyo kuhudumia mtanzania endapo utakipa mamlaka ya kushika dola kwa kuwapa wagombea wake kura nyingi za ndio katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
“Kama mwenyekiti wa chama cha Sauti Ya Umma (SAU), pamoja viongozi wenzangu wa chama chetu, tunayo dhamira ya dhati ya kuleta mabadiliko na maendeleo na kujenga mustakabali mzuri kwa wote.
“Sambamba na kulinda muungano wetu na kukuza umoja na mshikamano miongoni mwa watanzania na waafrika.
“Ilani hii ni zaidi ya hati ni ahadi. Ahadi ya kupigania haki zako na kufanya kazi bila kuchoka ili kuunda jamii yenye haki, jamii yenye maendeleo na jumuishi.”amesema Mpata
Hata hivyo Mpata amebanisha kuwa Ilani yao ni ramani ya mabadiliko wanayoyahitaji kwa pamoja na kupitia SAU wanaweza kushinda changamoto za leo na kujenga kesho iliyobora ambayo wote wanaweza kujivunia.
“Rai yangu, ninawaomba sana muungane nasi na mchukue maamuzi sahihi ya kuiamini na kuichagua kwa kura nyingi Chama cha Sauti ya Umma (SAU) ili kupata mustakabali bora kwa ajili yetu na kwa vizazi vijavyo”ameongeza Mpata
Katibu Mkuu wa SAU na Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majalio Kyara amesema amekuja kwa watanzania si tu kama mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini pia kama mtanzania anayeelewa changamoto zinazowakabili na kesho wanayoitamani.
“Nchi yetu imebarikiwa kuwa na ardhi yenye rutuba, raslimali nyingi na idadi nzuri ya vijana wanaotaka kuchangia maendeleo yetu ya pamoja.
“Hata hivyo, hatuwezi kupuuza hali halisi ya umaskini, ukosefu wa ajira na miundombinu duni ambayo inazuia ukuaji wetu.
“Nguzo zetu kuu za KILIMO, VIWANDA na TEKNOLOJIA katika ilani hii ya 2025 – 2030, zitawezesha kusukuma maendeleo, kudumisha jamii zetu, upatikanaji wa ajira na maendeleo kwa vijana wetu”amesema Kyara.
Kayra amebainisha kuwa wanatazamia taifa ambalo hakuna aliyesalia nyuma ambapo ndoto za vijana, hekima za wazee, na bidii za wakulima, wafanyakazi na wajasiriamali zinauungwa mkono.
Watanzania wanatarajiwa kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29,2025 na kuwachagua wagombea wa nafasi ya Urais,Ubunge na Udiwani watakaodumu kwa muda wa miaka mitano hadi 2030 utakapoitishwa uchaguzi mwingine.


Discussion about this post