NA MWANDISHI WETU,MOROGORO
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imewahimiza wafanyabiashara nchini kulipa kodi kwa hiari ili kuepuka riba na adhabu inayotozwa baada ya ucheleweshwaji wa malipo hayo
Wito wa umetolewa na Meneja wa TRA Wilaya ya Kilombero mkoani Mororogo Innocent Minja wakati awamu ya tatu ya kulipa Kodi ikitarajiwa kuhitimishwa Septemba 30,2025.
Hata hivyo Minja amewahimiza Walipakodi ambao bado hawajakamilisha malipo ya Kodi zao, kulipa kwa hiari ndani ya muda uliosalia.

Akizungumza na Walipakodi wakati wa zoezi la Elimu ya Kodi Mlango kwa Mlango lililoanza Septemba 26,2025.Minja amesema ni vema kila Mlipakodi akatimiza wajibu wake wa kulipa kodi kwa hiari ili kuepuka riba na adhabu inayotozwa baada ya kuchelewa kulipa Kodi.
Aidha Minja ameongeza kuwa malengo ya makusanyo yaliyowekwa na Serikali yatafikiwa iwapo kila mtu mwenye kipato atalipa kodi ambapo ndiyo maana TRA inaendesha zoezi la kutoa Elimu ya Kodi Mlango kwa Mlango.
Amefafanuwa kuwa wakati wa kutoa elimu pia wanatumia fursa hiyo kuwakumbusha Walipakodi kulipa Kodi ya awamu ya tatu ambayo inaishia Septemba 30,2025.
“Tunapita kutoa Elimu ya Kodi Mlango kwa Mlango kwa wafanyabiashara kwa lengo la kuwawezesha wanaotaka kulipa Kodi lakini hawajui mahala pa kuanzia kuanza kulipa Kodi jambo ambalo litaongeza wigo wa kodi” amebainisha Minja.

Baadhi ya Wafanyabiashara waliotembelewa wakizungumza kwa nyakati tofauti wameshauri zoezi hilo liwe endelevu na kuwapongeza TRA kwa kuwafuata na kuwapa elimu katika biashara zao.




Discussion about this post