• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Friday, December 5, 2025
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Siasa

CCM kukamilisha mchakato wa Katiba Mpya

Kuanzisha Ofisi ya Taifa ya Upelelezi

by bajeti
October 1, 2025
in Siasa
0
CCM kukamilisha mchakato wa Katiba Mpya

Mwenyekiti wa CCM na Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dkt Hussein Ali Mwinyi katika mikutano ya kampeni Visiwani Zanzibar.

Share on FacebookShare on Twitter

 

NA MWANDISHI WETU

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kinaamini kuwa misingi imara ya Utawala Bora, Demokrasia, Haki za Binadamu na Utawala wa Sheria ni muhimu katika kuhakikisha kuwa Taifa linaendelea kuwa na amani na utulivu.

Hata hivyo CCM kitaielekeza Serikali yake kuhuisha na kukamilisha mchakato wa katiba mpya.

Hayo ni kwa mujibu wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025  yenye kauli mbiu ‘’Kazi na Utu, Tunasonga Mbele’’  iliyotolewa Mei 2025 na kuzinduliwa Agost 28,2025 Kawe mkoani Dar es Salaam.

“Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 ni ahadi na mkataba mama kati ya CCM na Serikali yake na wananchi katika kipindi cha miaka mitano ijayo (2025 – 2030)”imeeleza Ilani hiyo

Ilani hiyo imebainisha kuwa CCM inaahidi kuendelea kuboresha uchumi, kuimarisha ustawi wa wananchi na kuhakikisha kuwa Serikali inayoiunda inaweka na kutekeleza mikakati thabiti ya kuinua hali za maisha za wananchi na kuboresha kipato chao.

“Lengo kuu la Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 ni kukuza uchumi na kuimarisha ustawi wa wananchi aidha, Ilani hii ni nyenzo ya CCM katika kuanza kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050”imefafanuwa Ilani hiyo

Katika Ahadi na Maelekezo ya CCM (2025 – 2030) ya Ilani hiyo,CCM imefafanuwa kuwa misingi imara ya utawala bora, demokrasia, haki za binadamu na utawala wa sheria ni muhimu katika kuhakikisha Taifa linaendelea kuwa na amani na utulivu.

“Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii, Chama kitaielekeza Serikali kuendelea kuimarisha demokrasia na utawala wa sheria kwa kutekeleza yafuatayo:

“Kuimarisha misingi ya demokrasia kwa kuboresha mazingira wezeshi ya wananchi kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii, kiuchumi na kisiasa kwa kuzingatia maadili na sheria za nchi.

“Kuhuisha na kukamilisha mchakato wa katiba mpya”imeongeza Ilani hiyo

Aidha CCM itaimarisha matumizi ya kamera za ulinzi (CCTV) na TEHAMA katika kubaini na kuzuia uhalifu na wahalifu.

“Kuanzisha mamlaka mpya na huru ya upelelezi inayojitegemea itakayojulikana kama Ofisi ya Taifa ya Upelelezi (National Bureau of Investigation) itakayokuwa na jukumu la kupeleleza makosa yote ya jinai.

“Kuboresha mishahara na maslahi ya askari wa Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, na uhamiaji ikiwamo kupitia upya umri wa kustaafu na mafao ya pensheni.”imebainisha Ilani hiyo

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM  na Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan,amesema Mwaka huu Taifa letu limetengeneza Dira mpya itakayoongoza mipango ya maendeleo ya nchi yetu kwa kipindi cha miaka 25 ijayo.

“CCM inaunga mkono matarajio yote yaliyoanishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, na tunaahidi kuyatekeleza kikamilifu.

“Ilani hii imezingatia kikamilifu maudhui na vipaumbele vilivyobanishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

“Kwa kipindi cha miaka mitano ijayo (2025-2030), CCM itaisimamia Serikali ili kuhakikisha kwamba tunaendelea kujenga uchumi imara, jumuishi na shindani; kulinda amani usalama na utulivu; na kuimarisha ustawi wa Watanzania kwa kuwawezesha kiuchumi na kufungua fursa zaidi za ajira na biashara.”amesema Rais Samia

Next Post
Serikali ya ADA-TADEA kuwalipa askari walioshiriki vita vya Kagera

Wanafunzi elimu ya juu kupigwa marufuku kupanga vyumba mtaani

Wamiliki wa  nyumba kuzuiwa kujenga frame za maduka katika maeneo ya makazi

Mradi wa Maji wa Miji 28 mkoani Niombe utakavyoondoa changamoto ya maji safi na salama

Mradi wa Maji wa Miji 28 mkoani Niombe utakavyoondoa changamoto ya maji safi na salama

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:46
  • Today's page views 46
  • Total visitors 12,087
  • Total page views 13,740

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In