NA GOODLUCK HONGO
TANZANIA imetajwa kuwa nchi ya tano duniani kwa kujenga Reli ndefu ya Kisasa ya (SGR) inayofikia zaidi ya kilomita 4000 nchi nzima ikitumia zaidi ya dola za kimarekani Bilioni 10.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa miradi mbalimbali inayoendelea kujengwa kwa sasa ya SGR katika maeneo tofauti nchini inayojumuisha kilomita zaidi ya 4000 na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya tano duniani kwa kujenga reli ndefu ya kisasa.
Hayo yamebainishwa katika kipindi cha maswali na majibu bungeni jijini Dodoma Januari 29,2026 katika Bunge la 13 Mkutano wa pili, Kikao cha tatu,Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile awakati akijibu swali na Mbunge wa Tabora Mjini Hawa Bananga.
Wakati Naibu Waziri Kihenzile akieleza hayo,Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) 2025-2030 kwa upande wa ahadi na maelekezo imebainisha kuwa Ujenzi wa miradi ya reli utapewa kipaumbele kwa reli ambazo zinafungua nchi kwa ajili ya biashara ili kutumia vizuri fursa ya kijiografia ambayo Tanzania inayo.
“Maelekezo ya CCM ni kutekeleza miradi ifuatayo katika kipindi hicho ni pamoja na Kukamilisha ujenzi wa reli ya SGR kwa kipande cha Mwanza – Isaka (km 341), Makutupora – Tabora (km 368), Tabora – Isaka (Km 165), Tabora- Kigoma (506), Uvinza- Musongati (km 156.6
Mbali na hilo lakini pia Ilani hiyo imebainisha kuanza ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Bandari ya Mtwara hadi Mbamba Bay na tawi lake kutoka Songea hadi Ludewa ili kuunganisha na mradi wa makaa ya mawe (Liganga) na madini ya chuma (Mchuchuma),
Ilani hiyo ya CCM imetaja sehemu nyingine kuwa ni pamoja na kujenga kipande reli ya kisasa (SGR) kutoka Itigi hadi Singida na kuanza ujenzi wa reli ya kisasa itakayounganisha Bandari ya Tanga kuelekea Arusha hadi Musoma (km 1,108) na itakayoungana na reli ya kisasa (SGR) ya kutoka Dar es salaam hadi Kigoma
“Hivi ninavyozungumza tayari Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameshaidhinisha fedha za kujenga reli kutoka Dar es Salaam Dodoma ambaye reli inafanya kazi,Dodoma mpaka Mwanza wakandarasi wako site(eneo la mradi),Tabora mpaka Kigoma wakandarasi wako site,tunakwenda mpaka sehemu ya pili ya nchi yetu ya nchi jirani kwa wenzetu Burundi.
“Niwahakikishie wananchi wote wanaodai fidia nchi nzima kwenye miradi ya reli wakiwemo wananchi wa Jimbo la Tabora Mjini kwamba tunakwenda kuwafikia na watupe muda kidogo wakati tunafanya chambuzi mbalimbali ili tuweze kuwafikia”amebainisha Kihenzile
Awali Mbunge wa Tabora Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Hawa Bananga alitaka kujua kuhusu kulipwa fidia kwa wananchi wa Jimbo la Tabora Mjini waliopisha ujenzi wa Reli ya Kisasa ( SGR) hususani kwenye Kata za Uyui na Ikomwa.




Discussion about this post