NA GOODLUCK HONGO
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Ayoub Mohamed Mahmoud amebainisha kuwa Wilaya 75 nchini hazina Vituo vya Polisi huku Kata 698 zikihitaji vituo hivyo kwa haraka kulingana na tathmini ya kina iliyofanywa na Jeshi la Polisi
Mbali na Wilaya hizo lakini pia Mikoa mitano haina Vituo vya Polisi Daraja A ikiwemo Kinondoni,Kanda Maalum ya Dar es Salaam na Morogoro
Mahmoud ameeleza hayo Januari 29,2026 Bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu katika Bunge la 13 Mkutano wa pili.
Amesema Kata 3471 sawa na asilimia 88 hazina vituo vya polisi ambapo Jeshi la Polisi lilifanya tathmini ya kina kuweza kufahamu hali halisi ya uhitaji lakini pia na matishio ya uhalifu kwa nchi nzima.
Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Simiyu kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Ester Midimu aliyehoji kuhusu Wilaya ya Maswa kutokuwa na Kituo cha Polisi,Naibu Waziri Mahmoud amemshukuru Mbunge huyo kwa swali lake zuri la msingi na kumpongeza kwa kuainisha changamoto katika Wilaya ya Maswa.
“Nataka nimjibu tu kwamba,Serikali ni kweli inafahamu kati ya Wilaya zilizopo nchi nzima hadi sasa tuna Wilaya 75 ambazo hazina vituo vya polisi.
“Na hili linatokana na kwamba ujenzi wa vituo vya Polisi unakwenda sambamba na kasi ya ukuaji wa uchumi na upelekaji wa maendeleo kwa wananchi katika maeneo mbalimbali.
“Na hili ni kweli Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Dkt.Samia Suluhu Hassan imefanya kazi kubwa mno na ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ya kuhakikisha kwamba barabara zinasogea karibu na wananchi ,vituo vya afya shule na kwa kufanya hivyo maana yake ukuaji wa uchumi wa watu lakini pia uhitaji wa ulinzi karibu na maeneo ya watu unazidi kukua”amesema Mahmoud
Amefananuwa kuwa katika hali hiyo mpango uliopo wa Wizara kupitia Jeshi la Polisi ni kuhakikisha kwamba wanakamilisha ujenzi wa Vituo vya Polisi vya Daraja A kwa maana vile vya Mkoa.
“Kwa sasa kuna mikoa mitano iliyobaki ambapo ni Mkoa wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Konondoni,Tanga Morogoro na Kagera.
“Kadhalika kukamilisha ujenzi wa Vituo vya Polisi katika ngazi ya Wilaya kikiwemo na hicho cha Wilaya ya Maswa ambavyo ni 75 kwa nchi nzima.
“Nikutoe hofu Mheshimiwa kadri ya hali ya fedha itakavyoruhusu tutahakikisha kwamba Wilaya ya Maswa nayo tunaijengea Kituo cha Polisi Daraja B.”ameeleza Mahmoud
Akizungumzia kuhusu Vituo vya Polisi vya Kata Naibu Waziri Mahmoud ameongeza kuwa hadi sasa wamebaini maeneo au Kata 698 kati ya 3147 zinauhitaji wa haraka wa upatikanaji wa vituo vya polisi baada ya tathmini ya kina kufanywa na Jeshi la Polisi .
“Kati ya Kata hizo 698 yako maeneo ambayo wananchi tayari wameanza kazi hiyo kwa kujenga maboma 77 ambayo maboma hayo ,jukumu lao kama Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Polisi ni kuhakikisha kwamba wanamaliza maboma hayo na kukamilisha vituo hivyo”amefafanuwa Naibu Waziri Mahmoud
Aidha ameongeza kuwa wakiweza kukamilisha maboma hayo 77watabakiwa na Kata 621ambazo zitahitaji ujenzi mpya wa vituo vya Polisi
“Mapango tulionao kama Serikali katika eneo hilo ni kuhakikisha kwamba wanagawa kazi hiyo katika awamu tatu,awamu ya kwanza tutaanza na vituo 196 ambavyo kati ya hivyo 77 ni kwa wale ambao wameshaanza hatua za awali za maboma 77
“119 tutaanza ujenzi upya na katika ujenzi huo wastani wa Sh.Bilioni 27.9zinahitajika kwa ajili ya ujenzi na ukamilishaji vituo hivyo”amesema Naibu Waziri Mahmoud
Ameongeza kuwa wanaamini wakianza awamu hii ya kwamba basi Mheshimiwa Salma Kikwete amekizungumzia basi watahakikisha nacho kinaingia katika mpango huo wa awamu ya kwanza.




Discussion about this post