• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Monday, May 11, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

‘Moto wa Waziri Mkuu Dkt.Nchemba waanza kuchoma’,Katibu Mkuu adaiwa kudhulumu Kampuni

Naibu Waziri TAMISEMI apigilia msumari

by bajeti
February 25, 2026
in Habari
0
‘Moto wa Waziri Mkuu Dkt.Nchemba waanza kuchoma’,Katibu Mkuu adaiwa kudhulumu Kampuni

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mwigulu Nchemba(Picha na OWM-TAMISEMI)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,ARUSHA

MOTO unaowashwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mwigulu Nchemba wa kusikiliza kero za wanachi katika ziara zake umeanza kuwagusa viongozi wa ngazi mbalimbali wanaodaiwa kupindisha haki za wananchi masikini.

Waziri Mkuu Dkt. Nchemba ambaye ameanza ziara katika mikoa ya Tanga na Kilimanjaro ambapo sasa yupo  mkoani Arusha akiendelea na ziara yake amekutana na makumi ya kero za wanachi hasa katika sekta ya elimu,ajira,mirathi,ardhi,malipo ya mishahara,dhuluma za nyumba,makampuni pamoja na unyanyasaji wa kujinsia.

Waziri Mkuu Dkt.Nchemba ambaye katika ziara yake hizo amekuwa akiongozana na baadhi ya mawaziri,timu za wanasheria,wabunge wa eneo husika pamoja na watendaji wa Taasisi za Serikali ambapo wakati mwinghine humlazimisha kuwainua ili kutolea ufafanuzi wa masuala ambayo wananchi wamekuwa wamekilalamikia.

Mfumo huo wa Waziri Mkuu Dkt. Nchemba wa kusikiliza kero mubashara  umewahamasisha wananchi wengi kujitokeza na kusababisha wengine kusafiri kwa kujigharamia nauli kutoka maeneo mbalimbali ya nchi ili kupata nafasi ya kusikilizwa  mbele ya Waziri Mkuu.

Hata hivyo katika hali isiyokuwa ya kawaida,Katibu Mkuu Mstaafu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Joyce Mapunjo amelalamikiwa kujimilisha Kampuni inayodaiwa kujihusisha na masuala ya utoaji wa (Msimbo Pau)Barcode

Akizungumza mbele ya Waziri Mkuu Nchemba Februari 24,2026 mkoani Arusha, mmoja wa wananchi aliyejitambulisha kwa jina la Jafari Juma amesema alianzisha wazo la biashara ya kutengeneza barcodes ndani ya Nchi ya Tanzania na kulipeleka kwa Wizara ya Viwanda na Biashara mwaka 2010.

Amesema Katibu Mkuu wa Wizara hiyo katika kipindi hicho alikuwa anaitwa Joyce Mapunjo ndiye aliyemdhulumu Kampuni yake na kujimilikisha.

“Kero yangu Mheshimiwa Waziri Mkuu,nilianzisha wazo la biashara la kutengeneza Barcodes ndani ya Nchi ya Tanzania,nilianzisha wazo 2010 na kupeleka barua katika Wizara ya Viwanda na Biashara.

“Katibu Mkuu wa wakati huo alikuwa anaitwa mheshimiwa Joyce Mapunjo alinidhulumu ile Kampuni mpaka leo na anaendelea kuiendesha na kujipatia  kipato kutokana na ubunifu wangu.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu nimehangaika sana katika kila eneo ili kupata haki yangu,hata mheshimiwa Mbunge wa Arusha Mjini Makonda anajua ni kwa kiasi gani nimehangaika kufuatilia suala hilo ili kuomba msaada huo.

Hata hivyo Juma amemthibitishia Waziri Mkuu Dkt Nchemba kuwa ana nyaraka zote za kuonesha uhalali wa yeye kubakia mmiliki wa Kampuni lakini wamemdhulumu,na kuongeza kuwa  Mwenyekiti wa Mkoa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) analielewa  suala lake.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu ninaomba uingilie kati pasipo wewe au Mama Samia sina uhakika kama nitapata haki yangu”amebainisha Juma

Mbali na hiklo lakini pia Juma licha ya kumueleza Waziri Mkuu Dkt Nchemba juu ya Kampuni hiyo lakini hakutoa ufafanuzi zaidi jinsi alivyodhulumiwa.

Akijibu lalamiko hilo,Waziri Mkuu Dkt.Nchemba alimtaka Juma kutoa maelezo hayo kwa wasaidizi wake aliokuwa nao katika eneo hilo ili waweze kuona namna ya kulishughulikia.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Dkt Jafar Seif amesema wanampongeza Waziri Mkuu Dkt. Nchemba kwa kazi kubwa anayoifanya kuanzia Mkoa wa Tanga,Kilimanjaro  na sasa Mkoa wa Arusha.

“Hakika Mheshimiwa Waziri Mkuu unarejesha tabasamu kwa watanzania na watanzania hawa wanakuamini na wanakupenda sana,na tunakuombea dua njema kwa Mungu.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu viongozi kama wewe ni nadra sana kuwapata na hawazaliwi kila mara,na maelekezo yako sisi kama TAMISEMI tumepaokea na tunaendelea kuyafanyia kazi.

“Hapa Arusha Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameelekeza zaidi ya Sh.Bilioni 30.6 ambazo zinakwenda kutekeleza miradi  mbalimbali ikiwemo ya Stand  na masoko”amesema Naibu Waziri Dkt. Seif

Hata Hivyo Naibu Waziri Dkt Seif amemuomba Waziri Mkuu Dkt.Nchemba kuendelea kuuwasha moto huo na wao kama TAMISEMI watatembea mguu kwa mguu kuhakikisha wanarejesha tabasamu la watanzania

Next Post
TFS na mikakati ya kulinda Mazao ya Misitu Kiteto

TFS na mikakati ya kulinda Mazao ya Misitu Kiteto

Bodi ya Maji Bonde la Pangani(PBWB) na mikakati ya kulinda,kuhifadhi vyanzo vya maji,yaonya watumiaji wasiona na  vibali

Bodi ya Maji Bonde la Pangani(PBWB) na mikakati ya kulinda,kuhifadhi vyanzo vya maji,yaonya watumiaji wasiona na vibali

Bodi ya Maji Bonde la Pangani(PBWB) na mikakati ya kulinda,kuhifadhi vyanzo vya maji,yaonya watumiaji wasiona na  vibali

Maji yaongezeka Bwawa la Nyumba ya Mungu,PBWB yahimiza wananchi kuchukua hatua

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:11
  • Today's page views 11
  • Total visitors 16,160
  • Total page views 18,327

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In