• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Saturday, July 11, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

EWURA yawahimiza wanahabari kuisemea jamii

Yasajili mafundi 270 wenye vipaji vya ufundi watakiwa kujiendeleza VETA

by bajeti
June 3, 2026
in Habari
0
EWURA yawahimiza wanahabari kuisemea jamii

Meneja wa EWURA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Walter Christopher akizungumza na waandishi wa habari Juni 2,2026 mkoani Njombe wakati wa mafunzo maalum yaliyoandaliwa na Mamlaka hiyo

Share on FacebookShare on Twitter

NA  MFAUME PASTORY,NJOMBE

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji  (EWURA) imewahimiza waandishi wa habari nchini kuwa mstari wa mbele katika kuisemea jamii kuhusu mambo yanayofanyika kinyume na utaratibu ili kuepusha madhara makubwa kutokea .

EWURA ambayo ni taasisi ya Serikali iliundwa mwaka 2001 kwa mujibu wa Sheria ya EWURA, Sura ya 414 ya Sheria za Tanzania na kuanza kazi Septemba 2006.

Madhumuni ya kuundwa EWURA ni kufanya udhibiti wa huduma za nishati na maji kwenye nyanja za kiufundi na kiuchumi za sekta ya nisahti na maji na usafi wa mazingira.

Hata hivyo EWURA inayoongozwa na Mkurugenzi Mkuu wake Gerald Maganga,kwa mujibu wa Kifungu cha 7 cha Sheria hiyo,kinaeleza majukumu ya Mamlaka hiyo baadhi yake yakiwa ni pamoja na kutoa, kuhuisha na kufuta leseni,kuweka na kusimamia viwango vya ubora wa huduma,kudurusu na kusimamia bei za huduma

Majukumu mengine ya EWURA ni pamoja na kutunga sheria ndogo na kanuni na kufuatilia maendeleo ya sekta zinazodhibitiwa kwa kuzingatia upatikanaji, ubora wa huduma, gharama ya huduma, ufanisi wa uzalishaji, uwekezaji na usambazaji wa huduma.

Meneja Mawasiliano wa EWURA Makao Makuu Wilfredy Mwakalosi akizungumza na waandishi wa habari Mkoa wa Njombe(hwapo pichani) Juni 2,2026 wakati wa mafunzo kwa wanahabari yaliyoandaliwa na Mamlaka hiyo.

 EWURA ambayo imekuwa na utaratibu wa kutoa taarifa mara kwa mara kuhusu huduma za nishaji na maji kwa wadau wake mbalimbali  ili kuwa na taarifa sahihi,imewahimiza pia waandishi wa habari,kuwa mstari wa mbele katika kuisemea jamii kuhusu mambo yanayofanyika kinyume na utaratibu ili kuepusha madhara makubwa kwa siku zijazo.

Wito huo umetolewa June 2,2026 mkoani Njombe na Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo Wilfredy Mwakalosi wakati  ikiwasilisha mada ya Kazi na wajibu wa Ofisi ya EWURA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini katika mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na Mamlaka hiyo kwa wanahabari ambao ni wanachama wa chama cha waandishi wa Habari Mkoa wa Njombe.

Mwakalosi amesema moja ya jukumu lao ni kuandaa na kuratibu mchakato wa kupata maoni ya wadau ambapo hapo ndipo eneo muhimu kwa wananchi kuelimishwa zaidi.

Aidha ameongeza kuwa waandishi wa habari wanapaswa kuwa sehemu ya kusaidia na  kuisemea jamii pindi wanapoona mtu anayetaka kufanya uwekezaji lakini anakiuka taratibu za kisheria kabla hajaendelea na uwekezaji kwani baadae huwa si rahisi kumwambia aondoe uwekezaji huo.

“Waandishi wasaidie kutoa elimu na kutoa maoni, mnapaswa kuwa kimbelembele kuiwakilisha jamii, mfano yale malalamiko ambayo yalikuwa yakitolewa na wananchi kuhusu utitiri wa vituo vya mafuta ni kwa sababu wananchi walikua wanaona ila walikuwa hawezi kuchukua hatua za kuwasilisha malalamiko mahala husika kwa wakati”

“Hili ni eneo muhimu ambalo wananchi wanapaswa kulizingatia na kuwa na uwezo wa kuchukua hatua za mapema kutoa taarifa kwa mamlaka husika na changamoto hii huwa si tatizo la Mamlaka yetu ya EWURA kwani sisi niwasimamizi wa huduma inayotolewa”amesema Mwakalosi

Waandishi wa habari Mkoa wa Njombe

Kwa upande wake Meneja wa EWURA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Ndugu Walter Christopher amesema wananchi wanapaswa kuangalia umbali wa eneo la uwekezaji na chanzo kilipo kwani kwa wastani inapaswa kuwa umbali wa mita 30 na kuendelea ndipo watu wanapaswa kufanya uwekezaji.

“Hii ndio sababu EWURA inaendelea kujenga na kuimarisha mahusiano yake na wadau na wananchi ili iwe rahisi kufikiwa na kushughulika na kero zote za wananchi.

“Tumekuwa  tukijenga mahusiano na wakuu wa wilaya kwa sababu wao wanafikishwa zaidi kero na wananchi na tumekuwa tukiwafikia wanahabari kwa kuwa ninyi mnauwezo mkubwa wa kuelimisha jamii ”ameeleza Christopher 

Christopher amebainisha kuwa EWURA inazalisha machapisho ambayo huelezea mambo muhimu na inafanya hivyo ili jamii iwe na uelewa yakiwemo mambo mbalimbali ambayo EWURA imekwisha yashughulikia na kuyapatia utatuzi.

Meneja wa EWURA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Walter Christopher akizungumza na waandishi wa habari( hawako pichani)Juni 2,2026 mkoani Njombe wakati wa mafunzo maalum yaliyoandaliwa na Mamlaka hiyo

Akizungumzia kuhusu vyanzo vya maji, Christopher   amefafanuwa kuwa mikoa ya kusini ina maji na maporomoka mengi ambayo  chanzo chake kikuu cha nishati ya umeme imekuwa ni maji.

 “Kanda nzima kwa sasa ina mafundi waliosajiliwa na EWURA zaidi ya 870 na kwa Mkoa wa Njombe pekee una mafundi zaidi ya 150.

“Tunawahimiza pia  mafundi ambao wamekuwa na vipaji vya ufundi umeme ila hawajasomea basi wakajiendeleze  Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) kwani Serikali imetoa fursa hiyo na kisha ,Mamlaka itawatambua na kuwapatia kibali cha kufanya kazi” ameongeza Christopher

Hata hivyo Christopher  amewahimiza  wananchi kuwatumia mafundi waliosomea na wenye vyetu vya EWURA ili kuepusha matatizo au majanga katika shughuli zao na makazi yao.

“Kutokana na utendaji bora wa EWURA imefanikiwa kupunguza kiwango kikubwa cha kupokea malalamiko.

“Kwa wastani sasa kwa mwezi tunaweza kupokea malalamiko mawili na yote yakashughulikiwa kwa ufanisi na pande zote husika zikaridhika kwa kuwa Mamlaka imekua ikihakikisha inatenda kwa usawa kwa wateja wake wote bila kuwa na upendeleo” amefafanuwa Christopher

Next Post
Kuelekea Dira ya Maendeleo 2050,Kuku wa nyama kuuzwa kwa uzito(kilo),’wafugaji wanukia utajiri’

Kuelekea Dira ya Maendeleo 2050,Kuku wa nyama kuuzwa kwa uzito(kilo),’wafugaji wanukia utajiri’

JET  yawataka waandishi wa habari kujikita katika uhifadhi wa maliasili,mapito ya wanyamapori(Shoroba)

Migongano baina ya binadamu na wanyamapori ni tishio kwa uhifadhi  endelevu

Matukio 1718 ya milipuko na moto hayajachunguzwa

Wajumbe wenye elimu darasa la saba wabainika Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tukuyu

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:122
  • Today's page views 122
  • Total visitors 20,836
  • Total page views 23,210

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In