• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Friday, July 10, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Sayansi na Teknolojia

Uzalishaji juisi ya ndizi utakavyoongeza ajira,soko la uhakika kwa wakulima

Utafiti wa Prof.Kibazoi waonesha ndizi zinaweza pia kutengeneza mvinyo

by bajeti
June 30, 2026
in Sayansi na Teknolojia
0
Uzalishaji juisi ya ndizi utakavyoongeza  ajira,soko la uhakika kwa wakulima

Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Prof.Oscar Kibazoi akionesha juisi aliyotengeneza kutokana na ndizi zenye utomvu mwingi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) walipomtembelea mkoani Dar es salaam hivi karibuni

Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO

UTAFITI wa Kilimo wa Mwaka 2022/23 Matokeo Muhimu uliotolewa Septemba 2025 na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) umeonesha kuwa Jumla ya tani Milioni  1.3 za ndizi zilizalishwa nchini Tanzania.

Kati ya kiasi hicho kilichozalishwa tani 1,352,281 zilizalishwa na kaya na tani 414 zilizalishwa kutoka mashamba makubwa ambapo Tanzania Bara ilizalisha  tani 1,294,765 huku Zanzibar ikizalisha tani 57,516

Ripoti hiyo inatoa takwimu muhimu za kilimo kutoka kwa wakulima wadogo katika ngazi ya kaya na mashamba makubwa kwa lengo la kuarifu sera za serikali, mipango, na program katika ngazi ya kitaifa na kimkoa.

Ndizi pia ni moja ya zao la chakula kama yalivyo mazao mengine lakini pia zao la biashara kwa wakulima wadogo na wakubwa.

Hata hivyo baadhi ya mikoa inayolima ndizi ni pamoja na Mbeya,Morogoro,Kilimanjaro na Mkoa wa Kagera ambapo ndizi  huzalishwa kwa wingi katika vijiji vya Mabira pamoja na Kamagambo katika Wilaya za Kyerwa na Karagwe.

Ndizi aina ya kali na kisukari na zingine ambazo kwa lugha ya Kabila la Wanyambo linalopatikana Wilaya ya Karagwe na Kyerwa huziita ebijoge na hutumika kutengeneza pombe inayojukana kama Rubisi  na juisi yake inayojulikana kama togwa(Omulamba).

Ndizi hizo huvundikwa hadi zitakapoiva na kisha kumenywa na kuwekwa kwenye kifaa kinachoitwa Obwato.

Baada ya kuwekwa kwenye Obwato ndipo zinaaanza kusagwa (Kujuungwa) kwa kutumia miguu ikichanganywa na majani ili zisiteleze hadi zitakapoanza kutoa juisi inayojulikana kama Omulamba (togwa) bila kuchanganywa na kitu kingine chochote.

Omulamba (togwa) ikishapatikana itachujwa ili kuondoa makapi na kisha kurudishwa kwenye Obwato kama ilivyokuwa awali na hapo ndipo linaweza kuuzwa ili watu waweze kunywa kama togwa(Omulamba).

Togwa hilo baada ya kupatikana na kuwa tayari kutumika,hufuatia hatua za utengenezaji wa pombe inayojulikana kama Rubisi.

Kwa upande wa utengenezaji pombe hiyo ya Rubisi,huchukuliwa Omulamba(togwa) lililo tayari kutumika na kisha kuchanganywa na Mtama uliokaangwa na kusagwa unga wake ndipo huvundikwa tena kama ilivyokuwa kwenye upatikanaji wa togwa.

Mchanganyiko huo huvundikwa kwa muda wa siku tatu ikiwa kwenye Obwato  na baada siku hizo ndio hutolewa na kisha kuchujwa kuondoa makapi na hapo ndipo pombe ya Rubisi inapopatikana.

Kutokana na mazingira ya utengenezaji wa juisi hiyo maarufu kama Omulamba kwa wakazi wa Kagera ulisababisha Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)Prof.Oscar Kibazoi kuamua kufanya utafiti katika kutengeneza juisi isiyo na kemikali kwa kutumia ndizi zenye utomvu mkali.

Anasema  kinywaji ni sehemu ya chakula na Tanzania bado inaagiza juisi kutoka nje ya nchi na pale wanapokunywa basi wanachangia kuzalisha ajira kutokana na uzalishaji kuongezeka.

Akizungumzia na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar es Salaam sababu za kufanya utafiti huo  miaka 20 iliyopita na kutoa matokeo yanayoweza kuzalisha makumi ya ajira kwa watanzania,Prof.Kibazoi anasema wakati alipomaliza Degree ya pili aliona jinsi togwa la ndizi linavyotengenezwa mkoani Kagera ambapo walitumia mikono na miguu.

Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Prof.Oscar Kibazoi akionesha mtambo wa kutengeneza juisi inayotakana na ndizi zenye utomvu mwingi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) walipomtembelea mkoani Dar es salaam hivi karibuni

Anasema  mkoani Kagera watu wengi wanalima zao la ndizi ili wale na sio kwa ajili ya fursa kama hizo hivyo wao waliangalia pia jinsi ya kuongeza thamani zao la ndizi.

Anasema baada ya kukanyaga ndizi hizo ili zilainike ndipo  hupatakana  togwa ambalo  likikaa siku tatu huzalisha pombe ya ndizi.

Anasema kilichosukuma zaidi kufanya utafiti  ni suala la usafi baada ya kuona jinsi wanavyotumia miguu na mikono kutengeneza togwa na alifanya utafiti kwa muda wa miaka mitatu ikiwemo kujua ukakasi wa ndizi na utomvu wake na faida zake kwa mwili wa binadamu.

Anasema baada ya utafiti huo ndipo walianza kusaga ndizi kwa kutumia mashine ndogo na kisha kutengeneza togwa la juisi ya ndizi bila kutumia mikono wala miguu.

“Ili utengeneze togwa(juisi) ya ndizi ni lazima upate ndizi yenye utomvu mkali au mwingi sana hivyo bila kuwa na ndizi yenye utomvu mwingi huwezi kutengeneza juisi hiyo.

“Ndizi ina madini mengi sana ikiwemo madini ya chuma hivyo tuliona kutengeneza juisi ya ndizi itasaidia hata afya kwa watanzania.

“Na faida ya juisi hii ya ndizi kwanza inaondoa kiu,kupata madini,sukari ambapo hupunguza kiwango hicho hadi kufikia asilimia 13 na hii ni juisi ya asili isiyo na kemikali yoyote ndani yake”anabainisha Prof.Kibazoi

Aidha anaongeza kuwa juisi hiyo inaweza kukaa zaidi ya mwaka mmoja bila kuharibika ambapo kwa sasa hawajanza kuzalisha kwa ajili ya biashara lakini wapo katika kutafuta uwezeshwaji ili kufungua kiwanda kikubwa cha kuzalisha juisi ya ndizi.

Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Prof.Oscar Kibazoi akionesha juisi aliyotengeneza kutokana na ndizi zenye utomvu mwingi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) walipomtembelea mkoani Dar es salaam hivi karibuni

Akizungumzia utafiti wake na Dira ya Maendeleo 2050,Prof.Kabazohi anasema teknolojia yao ya kutengeneza juisi ya  ndizi inaendana na Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050 inayotaka kufikia uchumi wa Sh.Trilioni moja.

“Tanzania tunaagiza sana juisi kutoka nje lakini hii juisi ni sehemu ya chakula hivyo watu wanapokunywa kwa wingi basi inachangia ajira katika mfumo wa uzalishaji kwa wingi”anaeleza Prof.Kabazohi.

Akizungumzia kuhusu elimu ya amali,Prof. Kibazohi anasema ni muhimu kuzidisha mafunzo kwa vitendo hasa kwa elimu inayohusu uhandisi ananainisha kuwa:

“Kwa upande wa kemia na usindikaji,tungeweza kuwa na fedha tungeweza kuwa na viwanda vidogo vidogo na sio vya matunda au mbogamboga tu hata vya kutengeneza mbolea kwa sababu tuna gesi asilia.

“Elimu hizi tumezipokea kutoka nje zimeletwa,sasa utafiti wangu umejikita katika mambo ambayo yapo hapa hapa nchini kwetu ambayo yanafaa kuendelezwa.

“Ukienda kwa mzungu ukimwambia hii ni juisi ya ndizi atashangaa sana,ingawa taratibu za sayansi au uhandisi ni zile zile; nadhani kuna haja ya kuangalia tunachomekaje masuala ya kwetu katika zile elimu”anaongeza Prof.Kibazoi

Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Prof.Oscar Kibazoi akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari na Maofisa waanndamizi kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) walipomtembelea mkoani Dar es salaam hivi karibuni

Prof.Kibazoi anabainisha kuwa watu wakitoka pale waende pamoja na mazoezi kuendeleza vya kwetu kwa sababu bila kuweka mle ndani na kuwafundisha tu kutoka nje hawana mahali pa kuviendelezea.

“Tunaweza tukaweka mitaala ambayo inaangalia huko na sio kununua mbolea kutoka nje na Serikali ikafadhili kununua mitambo ya kuendeleza na kuelekea huko na waanze kuwa wajasiriamali wa kutengeneza bidhaa. zinazotokana na malighafi zinazopatikana hapa nchini”anaongeza Prof.Kibazoi

Akizungumzia kuhusu uzalishaji wa ajira,Prof….anasema unaweza kuanza na ajira ya watu 10 kwa ajili ya uzalishaji na usambazaji lakini soko likiwa kubwa na ajira zitaongezeka zikiwemo za madereva,shambani na baadaye unaweza kufika hata watu 100.

“Mwanasheria au Mwandishi wa habari anapomaliza shule yeye anataka printa na kompyuta mapakato(laptop) tayari yupo kazini lakini Mwanasayansi na Mhandisi yeye anahitaji mitambo na wakati fulani tulifikiria kuwa na kiwanda kinachofanya kazi vizuri na tuligundua kuwa tunahitaji mitambo yenye gharama siyo chini na Sh.Bilioni moja na zaidi

“Lakini tumefupisha hapa kwenye hii Bilioni moja angalau tupate mahali pa kuanzia kwa sababu gani,Bilioni moja  haipo kwani ili uweze kumsimamisha mtoto mdogo aanze kutembea ni lazima kwanza awe anatambaa,kama hajaanza kutambaa huwezi kumshikilia asimame”anafafanuwa Prof.Kibazoi

Hata hivyo anabainisha kuwa wanahitaji fedha ili waanze kidogo kidogo katika hatua za uzalishaji ili mtoto atambae,asimame na ndipo awepo mtu wa kumfundisha kukimbia.

“Benki hawataki kesho wapate hasara,sio wamshikilie mtoto ambaye hajaanza kutambaa wanataka kumfundisha kutembea aanguke,wao wanataka kuona kwamba je mmeshaanza kuzalisha,unazalishaje,soko lako likoje hela zipo lakini mwanzoni lazima tubebwe bwebe kidogo ili tuweze kufika mahali”anasema Prof Kibazoi

COSTECH yaongeza nguvu

Akizungumzia kuhusu kukamilisha utafiti  wake,Prof.Kibazohi anasema walipata fedha ya awali na baadaye kupata fedha ya pili kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kiasi cha Sh.Milioni 100 ambapo baadhi ya fedha hizo zilisaidia kukamilisha utengenezaji wa juisi hizo zinazoonekana tayari.

“Kilichopo sasa hivi ni kutaka tuingie katika uzalishaji ambapo tutahitaji sehemu ya kuzalishia,mashine za kukamulia juisi,wataalam na  baada ya hapo tutaengeneza na mvinyo na hata pombe na vitu vingine.

“Ili uweze kutengeneza mvinyo unahitaji tunda lenye sukari zaidi ya asilimia 19,sasa sisi tunapata mpaka asilimi 28 ya sukari na inategemea aina ya ndizi hivyo ni rahisi kutengeneza mvinyo.

“Mwekezaji anayehitaji kuja basi tunamkaribisha”anabainisha Prof.Kibazoi

 

Next Post
DCEA yamnasa wakala wa dawa za kulevya Tanzania,yumo bibi wa miaka 70

Wanawake 46,464 wenye uraibu wa dawa za kulevya wapata tiba Vitengo vya Afya ya Akili.

Kamishna Jenerali Lyimo:Serikali hairogwi hata siku moja,yakamata boti,magari na ‘kuwapukutisha mapapa ‘wa biashara ya dawa za kulevya

Mali za Sh.Bilioni 3.3 yakiwemo 'majumba',magari yataifishwa,ni za wahalifu wa dawa za kulevya   

Rais Samia anavyoiheshimisha NHC,yaendelea kutimiza maono ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Rais Samia anavyoiheshimisha NHC,yaendelea kutimiza maono ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:391
  • Today's page views 393
  • Total visitors 20,702
  • Total page views 23,076

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In