• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Friday, July 10, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Wanawake 46,464 wenye uraibu wa dawa za kulevya wapata tiba Vitengo vya Afya ya Akili.

Muhimbili yaongoza kwa idadi kubwa,’Geita ngoma droo’

by bajeti
July 3, 2026
in Habari
0
DCEA yamnasa wakala wa dawa za kulevya Tanzania,yumo bibi wa miaka 70
Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO

HALI inatisha, hivyo ndivyo unavyoweza kusema juu ya maelfu ya wanawake wenye uraibu wa kutumia dawa za kulevya kupata tiba kwenye Vitengo vya Afya ya Akili dhidi ya wanaume.

Hata hivyo Kituo cha Afya ya Akili cha Muhimbili kinaongoza kwa kupokea idadi kubwa ya wanawake na wanaume waliofikia 31,468 huku wanawake wakiwa 23,232 na wanaume 8,231.

Hata hivyo moja ya sababu zinazochangia matumizi ya dawa za kulevya  ni pamoja na migogoro ya kifamilia  ambayo husababisha kukosekana kwa maelewano,upendo na mshikamano unaopelekea msongo wa mawazo unaotokana na ugomvi wa mara kwa mara,talaka,unyanyasaji au kutelekezwa.

Katika Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya   ya Mwaka 2025 iliyotolewa Mei 2026 na  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeleeza kuwa hali hiyo husababisha baadhi ya wanafamilia kutumia dawa za kulevya kama njia ya kukabiliana na changamoto hizo.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kuthibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania Aretas Lyimo

Aidha watoto wanaokulia katika familia zenye migogoro hukosa malezi bora na baadhi kukimbilia mtaani hivyo hushawishika kuingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya kwa urahisi.

Taarifa hiyo iliyowekwa saini na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera,Bunge ,Uratibu na Wenye Ulemavu) Prof.Palamagamba Kabudi na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)Aretas Lyimo imebainisha kuwa  idadi ya waliotibiwa Muhimbili inahusisha wale waliopewa rufaa kutoka vitengo vingine vya Afya ya Akili nchini.

“Watu wenye uraibu Mkoa wa Dar es Salaam walihudumiwa kwenye Vitengo vya Afya ya Akili vya Mwananyamala,Temeke na Amana.

“Muhimbili wanaume 8,231,wanawake 23,232 na jumla ni 31,463,Arusha wanaume 290,wanawake 1,653 na jumla ni 1943,Dar es Salaam(Mwananyamala,Temeke na Aman) wanaume 1490,wanawake 10,743 na jumla ni 12,172,Dodoma wanaume ni 669,wanawake 545 na jumla ni 1,214,Geita wanaume ni 130,wanawake 130 na jumla ni 260”imeeleza taarifa hiyo

Taarifa hiyo ya hali ya dawa za kulevya nchini kwa mwaka 2025 imebaiinisha mikoa mingine ikiwemo Iringa iliyokuwa na wanaume 75,wanawake 105 na jumla wakiwa 180,Kagera wanaume 203,wanawake 322 na jumla wakiwa 525,Katavi wanaume wakiwa 120,wanawake 95 na jumla wakiwa 215.

Mikoa mingine ambayo watu wenye uraibu walipata tiba kwenye Vitengo vya Afya ya Akili ni pamoja na Kigoma wanaume wakiwa 693,wanawake 635 na jumla wakiwa 1,328,Kilimanjaro wanaume ni 749,wanwake 832 na jumla wakiwa ni 1,581,Lindi wanaume ni 142,wanawake ni 113 na jumla wakiwa ni 255,Manyara wanaume ni 130,wanawake ni 251 na jumla kuu wakiwa ni 381,Mara wanaume ni 117,wanawake ni 153 na jumla ni 270.

Kwa upande wa Mkoa wa Mbeya wanaume ni 214,wanawake ni 271 na jumla ni 485,Morogoro wanaume ni 605,wanawake ni 531 na jumla ni 1,136,Mtwara wanawake ni 163,wanaume ni 142 na jumla ni 305,Mwanza wanaume ni 360,wanawake ni 1,604 na jumla ni 1,964.

“Njombe wanaume ni 98,wanawake ni 109 na jumla ni 207,Pwani wanaume ni 417,wanawake ni 2,895  na jumla ni 3,312,Rukwa wanaume ni 144,wanawake ni 108 na jumla ni 252,Ruvuma wanaume ni 269,wanawake 255 na jumla ni 524,Shinyanga wanaume 179,wanawake 161 na jumla ni 340,Simiyu wanaume ni 151,wanawake 140 na jumla ni 291,Singida wanaume ni 77,wanawake ni 148 na jumla ni 225,Songwe wanaume ni 168,wanawake ni 193 na jumla ni 361,Tabora wanaume ni 294,wanawake ni 221 na jumla ni 515,Tanga wanaume ni 345,wanawake ni 877 na jumla ni 1,222.

“Jumla kuu wanaume ni 16,462, wanawake ni 46,464 na jumla ni 62,926”imeongeza taarifa hiyo.

Next Post
Kamishna Jenerali Lyimo:Serikali hairogwi hata siku moja,yakamata boti,magari na ‘kuwapukutisha mapapa ‘wa biashara ya dawa za kulevya

Mali za Sh.Bilioni 3.3 yakiwemo 'majumba',magari yataifishwa,ni za wahalifu wa dawa za kulevya   

Rais Samia anavyoiheshimisha NHC,yaendelea kutimiza maono ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Rais Samia anavyoiheshimisha NHC,yaendelea kutimiza maono ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:391
  • Today's page views 393
  • Total visitors 20,702
  • Total page views 23,076

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In