• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Sunday, October 18, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Askofu Gwajima: aliyewapeleka waumini wetu mahabusu wametoka na hawaogopi mabomu ya machozi

Asema mahala ambapo hapana haki kwenye jengo la Kanisa lake haki itakapatika

by bajeti
October 17, 2026
in Habari
0
Askofu Gwajima: aliyewapeleka waumini wetu mahabusu wametoka na hawaogopi mabomu ya machozi

Kiongozi Mkuu na mwanzilishi wa makanisa ya Ufufuo na Uzima duniani Askofu Josephat Gwajima (wa tatu kutoka kulia) akikata utepe kuzindua Jengo jipya la kanisa hilo Oktoba 16,2026 Ubungo mkoani Dar es Salaam

Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO

ASKOFU na Kiongozi Mkuu na mwanzilishi wa makanisa ya Ufufuo na Uzima duniani Josephat Gwajima amesema  aliyewapeleka mahabusu waumini wa kanisa hilo amewafundisha vita na wametoka hawaogopi washawasha wala mabomu ya machozi bali wanamuogopa mungu  auaye mwili na roho.

Askofu Gwajima ametoa kauli hiyo Oktoba 16,2026 jijini Dar es Salaam mbele ya maelfu ya waumini wake wakati akizindua jengo jipya la Kanisa hilo aliloiita hekalu baada ya kukamilika kwa ujenzi wake uliochukua zaidi ya miaka mitatu.

Amesema ukimpekea mtu wa mungu gerezani huwa anakwenda na neno lake gerezani na ukimpeleka mtu wa mungu selo,umempeleka mwinjilisti selo.

“Kwa mara ya kwanza waumini wetu na wanangu waliingia mahabusu na wakaimba,wakaomba na wakamshukuru mungu  na wala hawana uchungu leo,mawazo yao ni kwamba aliyewapeleka kule aliwafundisha vita na wametoka kule hawaogopi washawasha,hawaogopi mabomu ya machozi lakini wanamuogopa mungu yeye auaye mwili na roho pia.

“Leo tunaweka wakfu hekalu hili jipya lakini mungu anatuuliza swali kubwa sana leo,hekalu hili litatumika kwa ajili ya kusudi gani.

“Ninaomba kila mtu afahamu,kwanza maombi yasiyokoma,ninaombi maombi yasikome katika nyumba hii,ninaomba kizazi baada ya kizazi kiingie katika uwepo wa mungu hapa,ninaomba wachungaji waombe hapa,waumini waombe hapa ,vijana waombe hapa,watoto waombe hapa na moto wa maombi usizimike kamwe”amesema Askofu Gwajima

Askofu Gwajima ameeleza kuwa anaomba pia mahali hapo pawe ni nyumba ya watu kupona,kurudishwa ,kufunguliwa,kufufuliwa na kupata maana ya matumaini ya maisha mapya waliyoyapoteza leo na kizazi kijacho

Amebainisha kuwa nyumba hiyo ni lazima iwe nyumba ya utume kwa mataifa yote na kuomba injili inayotokea katika nyumba hiyo iende Tanzania kote,Afrika Mashariki,Afrika na mataifa duniani kote

Gwajima ameongeza kuwa kila mtu atakayefika katika hekalu hilo asiishie kushangazwa na ukubwa na uzuri wa jengo hilo bali akutane na Yesu Kristo aliyefufuka kwa wafu na amjue mungu na maisha yake yastawi

“Kwa hiyo kazi ya jengo hili si tu kuabudu,kuombea wagonjwa bali pia ni kisima cha haki,mahala ambapo hakuna haki kwenye jengo hili haki itapatikana.

“Narudia tena mahala ambapo hapana haki kwenye jengo hili haki itakapatika.amesema Gwajima

Gwajima amebainisha kuwa Yesu alipokufa msalabani alizikwa,akakaa siku tatu na siku ya tatu akafufuka kutoka kwa wafu,akawaambia wanafunzi wake amani iwe pamoja nanyi,amani nawapa,amani nawaachia,sio kama ulimwengu utoavyo,msiwe na shaka mioyoni mwenu.

Katika uzinduzi wa Kanisa hilo,makumi ya waumini waliofurika kushuhudia uzinduzi huo walishiriki kwa pamoja chakula zikiwemo nyama choma.

Next Post
Joseph Kabila,Rais Mstaafu wa Kongo, uliyewafanyia mema wakongo,shukrani yao ni kumhukumu kifo,na kumfilisi mali zake

Joseph Kabila,Rais Mstaafu wa Kongo, uliyewafanyia mema wakongo,shukrani yao ni kumhukumu kifo,na kumfilisi mali zake

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:2
  • Today's page views 2
  • Total visitors 22,590
  • Total page views 25,184

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In