• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Tani bilioni 8.5 za barafu zayeyuka baada ya joto kuongezeka Greenland.

by BAJETI
August 1, 2021
in Mazingira
0
Share on FacebookShare on Twitter

JOTO kali lililorekodiwa Greenland ya Mashariki limesababisha tani bilioni 8.5 za barafu kuyeyuka na kuingia baharini ndani ya siku moja.

Mbali na tani hizo tayari ongezeko la joto katika maeneo mbalimbali duniani limeua makumi ya watu ambapo nchini Canada pekee idadi ya walikufa kutokana na joto kali wamefikia zaidi ya  800.

Hata hivyo Japani nayo imetangaza  vifo vya watu 23 vilivyosababishwa na ongezeko la viwango vya joto

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na Shirika la Habari la Uturuki jana limeeleza kuwa  data zilizotolea nchini Denmark zimefafanua kuwa tani bilioni 8.5 za barafu ziligeuka maji katika siku moja tu huko Greenland.

.Kulingana na taarifa hiyo ya Denmark, zaidi ya tani bilioni 100 za barafu zimeyeyuka na kutoweka huko Greenland tangu mwezi Juni 2021.

Kiwango cha barafu kinachoyeyuka huchanganyika na maji ya bahari, na kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha maji baharini.

Kulingana na utafiti wa 2019, kuyeyuka kwa barafu huko Greenland kunaweza kusababisha viwango vya bahari kuongezeka kati ya sentimita tano na 33 mwishoni mwa karne hii

Awali kulingana na Huduma ya Hali ya Hewa ya Canada, joto la nyuzi 46.1 lililorekodiwa katika jimbo la British Columbia na kurekodiwa kama joto la juu kabisa kuwahi kutokea nchini humo.

Rekodi ya awali ya joto la juu katika historia ya nchi hiyo ilikuwa nyuzi 45 Celsius, iliyorekodiwa katika jimbo la Saskatchewan mnamo Julai 1937.

Wakati joto hilo likiongezeka,imeripotiwa kuwa theluji iliyeyuka haraka zaidi ya inavyotarajiwa kwa sababu ya joto hilo, ambapo nyumba nyingi zimehamishwa kutokana na kuongezeka kwa viwango vya maji katika mto.

Wakati huo huo nchini Ugiriki ongezelo la joto limesabaisha kuzuka kwa moto katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.

Shirika la Hali ya Hewa duniani (WMO) iliulelezea mwaka 2019 kama mwaka uliokuwa na joto kali zaidi duniani baada ya mwaka 2016.

Next Post

Joto kali latishia uhai wa maelfu ya watu barani Ulaya

Dkt. Kalemani awaonya wakandarasi umeme wa REA

Majimbo 35 yakumbwa na moto unaosababishwa na ongezeko la joto Uturuki

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In