• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Majimbo 35 yakumbwa na moto unaosababishwa na ongezeko la joto Uturuki

by BAJETI
August 3, 2021
in Mazingira
0
Share on FacebookShare on Twitter

UTURUKI imesema kuwa moto wa msituni uliowaka katika majimbo 35 ya nchi hiyo umedhibitiwa lakini vita dhidi ya kupambana na janga hilo inaendelea.

Hali hiyo inatokana na joto kuongezeka katika viwango vya juu katika baadhi ya nchi za Bara la Ulaya,America na Asia kutokana nakile kinachoelezwa na wataalamu kuwa ni mabadiliko ya tabianchi na kupelekea misitu kuwaka moto na barafu kuyeyuka kwa kasi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Nchi hiyo (TRT), Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Fahrettin Altun, alitoa taarifa hiyo akisema kuwa vita dhidi ya moto wa misitu ulioathiri nchi hiyo inaendelea kwa kuhamasisha njia zote za serikali.

“Moto 122 kati ya 129 katika majimbo 35 yamedhibitiwa.”amesema Altun

Awali Julai 31,2021 Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan alifanya mazungumzo ya simu na Rais wa Urusi Vladimir Putin juu ya mambo mbalimbali ikiwemo moto.

Kulingana na taarifa iliyoandikwa na kutolewa na Ikulu ya Rais wa Urusi (Kremlin), moto wa misitu nchini Uturuki ulijadiliwa katika mazungumzo ya simu kati ya Rais  Erdoğan na Rais Putin.

Rais Erdoğan alimshukuru Rais Putin kwa kutoa ndege tano za kuzima moto na helikopta tatu zaidi kusaidia vita vya Uturuki dhidi ya moto unaowaka katika misitu ya nchi hiyo unaosababishwa na ongezeko la joto.

Rais Putin alisisitiza kuwa wataendelea kuisaidia Uturuki katika kuzima moto huo.

Next Post

Afungwa maisha kwa kumlawiti mtoto wa miaka tisa

TAG yawataka waumini kuongeza maombi ili kuleta umoja katika jamii

Makalla:Tutaigaragaza Azam Media

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In