MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amesema wataigaragaza timu ya mpira wa miguu ya Azam Media watakapokutana siku ya Agosti 14 mwaka huu katika viwanja vya Jeshi Masaki.
Mbali na hilo lakini pia Makalla amedhamiria kuipandisha daraja timu ya Masaki ili iweze kushiriki michuano mbalimbali na ligi za ngazi ya juu.

Akizungumza wakati wa mazoezi na timu hiyo, mkoani Dar es Salaam leo,Makalla amesema licha ya kujipanga kuipandisha daraja timu hiyo ya Masaki lakini pia ni muhimu kwa wananchi kufanya mazoezi ili kuimarisha Afya zao na kukabiliana na magonjwa hususani Uviko-19(CORONA).
“Nikiwa kama mlezi nimedhamiria kuipandisha daraja timu ya Masaki na kuhakikisha inashiriki michuano mbalimbali na ligi za ngazi ya juu ambapo kutakuwa na Timu ya Masaki Vijana na Masaki Veterans”amesema Makalla.
Makalla amebainisha kuwa Agost 14 mwaka huu timu hiyo ya Masaki ambayo yeye ndio Mwalimu anayeifundisha itashuka dimbani kuikabili timu ya Azam Media na kubainisha kuwa wataigaragaza mapema katika Uwanja wa Jeshi Masaki .
Hata hivyo licha ya kuifundisha timu hiyo na kushiriki nayo mazoezi,Makalla ametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya michezo ikiwemo Jezi, Mpira na Vifaa vya kufundishia kwa timu hiyo ya Masaki.
Makalla amewataka wananchi kufanya mazoezi katika kipindi hiki cha ugonjwa wa Uviko-19(CORONA) na magonjwa yasiyoambukiza ili kuimarisha afya zao..
Discussion about this post