• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Afungwa maisha kwa kumlawiti mtoto wa miaka tisa

by BAJETI
November 16, 2023
in Habari
0
Share on FacebookShare on Twitter

MKAZI wa Yombo Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam,Lukuman Ally amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya Mahakama ya Wilaya Temeke kumkuta na hatia kwa kosa la kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka tisa.

Inadaiwa kuwa mwezi  Mei mwaka 2020 maeneo ya Yombo njia panda ya Mwinyi Wilaya ya Temeke mshtakiwa huyo alimlawiti mtoto huyo huku akijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria. 

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi,Jimson Mwankenja ambapo amesema mahakama hiyo imejiridhisha na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka hasa mtoto aliyefanyiwa kitendo  hicho.

Mwankenja amesema alipopitia ushahidi hasa wa mtoto mwenyewe mahakama hiyo imeridhika kuwa mshtakiwa alifanya tendo hilo hivyo inamtia hatiani .

“Jamhuri ilileta mashahidi watano ambao ni mama mzazi wa mtoto huyo,Daktari wa Hospitali ya Mkoa wa Temeke,Emanuel Shija,Mwalimu wa Shule,mpelelezi wa Kituo cha Polisi Chang’ombe,WP3515 Catherine ,mhanga mwenyewe na kielelezo kimoja cha PF3 huku mshtakiwa akijitetea mwenyewe “amesema Mwankenja.

Amesema mtoto huyo wakati anafanyiwa tendo hilo alikuwa darasa la tatu na alikuwa anaishi na mama yake ambapo walikuwa wamepanga nyumba moja na mshtakiwa huyo.

Mwankenja ameongeza kuwa mshtakiwa huyo alikuwa na tabia ya kupika wali na kuwaalika watoto wote wa wapangaji kula nao chakula ndani na wakishamaliza anawatoa huku akimbakisha ndani  mtoto huyo peke yake na kuanza kumfanyia vitendo hivyo.

“Kwa maelezo ya mtoto amedai alimfanyia vitendo hivyo mara nne na hakuweza kumwambia mama yake kutokana alikuwa mkali hata hivyo aliyegundua Mwalimu wake  alivyokuwa akitembea na anavyokaa  akamuuliza na kumjibu ni  uncle Lukuman amekuwa akimlawiti”amesema Mwankenja

Hakimu Mwankenja amefafanua kuwa Mahakama hiyo baada ya kuangalia kifungu cha 154(2) cha kanuni ya adhabu,uzito wa kosa,maslahi ya umma,maslahi ya mshtakiwa mwenyewe,uwepo wa kosa la ulawiti katika Wilaya hiyo na shufaa zilizowasilishwa  na Wakili wa Serikali hivyo Mahakama inakupa adhabu ya kifungo cha maisha jela”amesema Mwankenja 

Awali Wakili wa Serikali,Anna Chimpaya aliiomba Mahakama hiyo itoe adhabu kali kwa mshtakiwa huyo kwa kuwa vitendo hivyo vimekuwa vikiongezeka katika Wilaya hiyo.

 

Next Post

TAG yawataka waumini kuongeza maombi ili kuleta umoja katika jamii

Makalla:Tutaigaragaza Azam Media

Moto wakimbiza maelfu ya watu Ugiriki

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:9
  • Today's page views 9
  • Total visitors 13,065
  • Total page views 14,810

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In