• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Sayansi na Teknolojia

Makalla amshukuru Rais Samia kuongeza bajeti ya TARURA

by BAJETI
August 10, 2021
in Sayansi na Teknolojia
0
Share on FacebookShare on Twitter

BAJETI ya Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA) imepanda kutoka Sh. Bilioni 25 hadi kufikia kiasi cha Sh.Bilioni 40 kwa Mkoa wa Dar es Salaam huku kitaifa ikifikia Sh.Bilioni 300.

Kauli hiyo imetolewa leo mkoani Dar es Salaam na Mkuu wa Mkoa Amos Makalla wakati wa utilianaji sahini awamu ya kwanza ya mikataba 41 yenye thamani ya Sh. Bilioni 14.1 kwa ajili ya ujenzi wa Barabara za Mkoa wa Dar es salaam.

Amesema anamshukuru na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza bajeti ya barabara za TARURA nchi nzima hali itakayosaidia uboreshwaji wa barabara za vijijini.

“Ninafurahishwa na ongezeko la bajeti ya Ujenzi wa Barabara Dar es salaam kutoka Sh. Bilioni 25 hadi Sh.Bilioni 40 na kwa nchi nzima kufikia Sh.Bilioni 300.

Makalla amesema mafanikio hayo yote ni matokeo ya kazi kubwa na nzuri ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan Katika utatuzi  wa kero za wananchi.

Aidha RC Makalla amewaelekeza Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA),Wakala wa Barabara nchini(TANROADs), Wakala wa Barabara Vijijini(TARURA), Shirika la Mawasiliano Tanzania(TTCL) na Shirika la Umeme nchini(TANESCO) kufanya kazi kwa pamoja ili kuondoa tatizo la miradi kutomalizika kwa wakati Kutokana na taasisi husika kuchelewa kuhamisha miundombinu.

Hata hivyo Makalla amewaelekeza TANROADs na TARURA kuhakikisha wanasimamia utunzaji wa miundombinu ya barabara ikiwa ni pamoja na usafi, ukarabati na uwekaji wa vibao vya kuzuia biashara kwenye eneo la hifadhi ya barabara. Makalla amewahimiza  wakandarasi wote waliosaini mikataba hiyo kuhakikisha wanakamilisha miradi kwa wakati na kwa viwango vinavyohitajika.

Next Post

Ongezeko la joto laendelea kusababisha vifo duniani

Ongezeko la joto laitesa Canada

Moto waibukia Ufaransa,maelfu ya watu wahamishwa

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:5
  • Today's page views 5
  • Total visitors 13,061
  • Total page views 14,806

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In