• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Zambia kujenga bomba la kisasa kusafirisha mafuta

by bajeti
July 5, 2022
in Habari
0
Zambia kujenga bomba la kisasa kusafirisha mafuta

Bomba la mafuta

Share on FacebookShare on Twitter

LUSAKA ,ZAMBIA

ZAMBIA imesema itaanza ujenzi wa bomba la mafuta lenye urefu wa Km. 700 sawa na maili 435 ili kuingiza mafuta ya dizeli kutoka nchini.

Ujenzi huo ambao utafanyika kwa awamu tatu utagharimu dola za kimarekani Milioni 300 katika ujenzi wa awali.

Waziri wa Nishati wa Zambia Peter Kapala ametoa kauli hiyo Juni 3,2020 na kuongeza  kwamba bomba hilo jipya litaenda sambamba na la sasa lakini litakuwa la kisasa zaidi.

“Baada ya miezi michache, bomba litaanza kusukuma mafuta ya dizeli nchini Zambia kutoka Tanzania”amesema Kapala

Amesema awamu ya kwanza ya bomba hilo itaishia Mpika (Wilaya ya Kaskazini mwa Zambia), awamu ya pili Ndola (Mkoa wa Copperbelt) na awamu ya tatu Solwezi (kaskazini magharibi mwa Zambia),”

Hata hivyo,Kapala  hakutoa maelezo zaidi kwa awamu ya pili na ya tatu ya mradi huo.

Ujenzi wa bomba hilo unakuja wakati ambapo Serikali kwa kushirikiana na nchi ya Zambia  wanatumia bomba la mafuta la TAZAMA, lenye urefu wa Km 1,710 sawa na maili 1,063 kusafirisha mafuta ghafi ya petroli kutoka bandarini hadi katika Kiwanda cha Kusafisha Petroli cha Indeni kilichopo  Ndola, Zambia.

Aidha Kapala amesema bomba la dizeli, ambalo litakuwa na ubora wa hali ya juu zaidi kuliko TAZAMA, litakuwa muhimu katika malengo ya muda mrefu ya nchi hiyo ya kuleta utulivu wa usambazaji wa dizeli ikiwemo kudumisha bei nzuri ya reja reja.

Matumizi ya sasa ya dizeli ya kila siku nchini Zambia yanakaribia lita milioni mbili, huku watumiaji wakuu wakiwa migodini, na kiwango cha usambazaji wa bidhaa nchini humo kimesalia kuwa salama licha ya changamoto za vita nchini Ukraine na Urusi.

mwisho

 

Next Post
Maendeleo Sekta ya Gesi na Mafuta kusaidia miradi ya kimkakati

Maendeleo Sekta ya Gesi na Mafuta kusaidia miradi ya kimkakati

SMT:Ukosefu wa nidhamu unasababisha miradi kutokalimika

SMT:Ukosefu wa nidhamu unasababisha miradi kutokalimika

Wanahabari:Bodi ya Ithibati  ya Habari iundwe na wanataaluma husika.

Wanahabari:Bodi ya Ithibati ya Habari iundwe na wanataaluma husika.

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In