NA GOODLUCK HONGO,PWANI
MWENYEKITI wa Shirika la Maendeleo na Utunzaji wa Mazingira (SMT) Mkoa wa Pwani, Augustino Noto amesema nidhamu ndio jambo muhimu katika kufikia malengo kwa kuwa sheria hazipo serikalini pekee bali hata kwa mashirika binafsi.
Hata hivyo Noto ameongeza kuwa miradi mingi inashindwa kufanikiwa kutokana na kukosekana kwa nidhamu za viongozi na wafanyakazi kwa kuwa hawakosi visingizio pindi mambo yanapoharibika
Noto ametoa kauli hiyo juzi wilayani Mkuranga mkoani Pwani wakati akizungumza na wakuu wa idara mbalimbali wanaohudumu chini ya ofisi yake.
Amesema Ofisi hiyo ya Mkoa ina jumla ya wafanyakazi 25 wakiwemo wakuu wa idara za Habari,Mazingira,Mipango na Fedha Elimu na zingine ambapo kazi kubwa walizonazo ni kuhakikisha mkoa huo kupitia SMT, unafanya vizuri katika suala la mazingira.
“Ni lazima tuwe na nidhamu katika kutekeleza majukumu yetu wote ili kufikia malengo tuliyojiwekea katika kufanikisha malengo ya miradi iliyopo ili kuleta tija kwa wananchi na serikali kwa ujumla,”amesema Noto

Noto amebainisha kuwa mazingira ndio kipaumbele cha SMT hivyo kila mwana SMT ni muhimu kuhakikisha kuwa mazingira yanalindwa katika eneo lake ili kuisaidia serikali na wananchi.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa SMT Mkoa wa Pwani John Naggar, amesema SMT Mkoa wa Pwani inahudumia halmashauri tisa ikiwemo Mkuranga,Kisarawe,Rufiji,Kitibi,Kibaha Mjini,Bagamoyo,Chalinze hivyo kila mkuu wa idara ngazi ya mkoa na kazi kubwa ya kufanya ndani ya halmashauri hizo.
Naye Naibu Katibu wa SMT Mkoa wa Pwani Geofrey Katunzi, amewataka wakuu hao wa idara kukufanya vikao vya mara kwa mara na wenzao ngazi ya wilaya ili kufikia malengo na mikakati ya shirika hilo.
mwisho




Discussion about this post