• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Watafiti sekta ya uvuvi watakiwa kuibua fursa

by bajeti
July 13, 2022
in Habari
0
Watafiti sekta ya uvuvi watakiwa kuibua fursa

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na Watafiti wa masuala ya Uvuvi (hawapo pichani)kutoka Tanzania na Nje ya Nchi katika mkutano wa mwaka wa kisayansi uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.(Picha na mpigapicha wetu)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewataka watafiti katika Sekta ya Uvuvi kujikita katika kuibua fursa zinazopatikana kwenye uchumi wa buluu ili ziweze kuvutia wawekezaji na kuinufaisha jamii.

Ulega ameyasema hayo katika Mkutano wa Mwaka wa Kisayansi uliowakutanisha watafiti mbalimbali wa masuala ya uvuvi uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.

Amesema kuwa baharini kuna mazao mbalimbali ambayo yanaweza kusaidia jamii kupata kipato na kuvutia uwekezaji mkubwa.

“Dunia kwa sasa inaelekea kwenye uchumi wa buluu, kuhakikisha rasilimali maji zinatumika ipasavyo kwenye kumsaidia mwanadamu na watafiti wana nafasi kubwa kwa sababu  kupitia tafiti zao wanaweza kuibua fursa na changamoto zilizopo katika eneo hilo ’’amesema Ulega

Aidha Ulega ameongeza kuwa  watafiti ni muhimu wakatumia taaluma zao kwa kushirikisha jamii inayonufaika na tafiti wanazofanya ili  kuweza kuionesha dunia fursa zilizopo kwenye sekta ya uvuvi kwa lengo la kuvutia wawekezaji wengi zaidi.

“Upande wa baharini tuna  Mwani, Majongoo bahari na Kaa, upande wa maziwa tuna  Sato, Sangara na Dagaa, haya yote ni mazao na yakielezwa vizuri na uwekezaji ukapatikana itainua uchumi wa watu wetu,” amebainisha Ulega

“Watafiti wakiibua fursa hizo na kuvutia wawekezaji itakuwa inaenda sambamba na malengo na nia ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kualika uwekezaji kwenye sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya uvuvi kwa maendeleo ya nchi na Taifa kwa ujumla.

Mkutano huo wa Mwaka wa Kisayansi  unafanyika kwa siku tatu kuanzia Julai 12 hadi 14 na  umekutanisha watafiti wa masuala ya uvuvi kutoka ndani na nje ya nchi kwa lengo la kujadiliana na kubadilishana mawazo juu ya namna ya kufanya ili uchumi wa buluu hasa upande wa sekta ya uvuvi kuwa endelevu.

 

Next Post
Kambole:Makosa tasnia ya habari yasiwe kosa la jinai

Kambole:Makosa tasnia ya habari yasiwe kosa la jinai

Nape awatoa hofu wanahabari

Nape awatoa hofu wanahabari

Sabasaba

Sabasaba

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In