• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Kambole:Makosa tasnia ya habari yasiwe kosa la jinai

by bajeti
July 13, 2022
in Habari
0
Kambole:Makosa tasnia ya habari yasiwe kosa la jinai

Waziri wa Katiba na Sheria Dk.Damas Ndumbaro

Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO

 

WAKILI Msomi Jebra Kambole amesema mabadiliko yoyote yanayotakiwa kufanyika katika  sheria mbalimbali ikiwemo ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 ni muhimu kuwashirikisha wadau wote ili kutorudia makosa yaliyopita.

Kauli ya Wakili Kambole imekuja siku chache wakati wadau wa habari wakiendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha kuwa vifungu vya sheria vinavyoonekana kukandamiza tasnia ya habari vinafanyiwa marekebisho.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo juu ya Sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016 na ile ya Makosa ya Mtandaoni ya 2015, Kambole amesema makosa yote yanayofanywa na waandishi wa habari yanapaswa kuwa ni makosa ya kimaadili na isiwe kosa la jinai linalopelekea vifungo.

Ameeleza kuwa  Sheria hiyo inakikuka Mkataba wa Kimataifa na ule wa Afrika Mashariki katika Ibara ya 7(b) ambapo wadau wa habari ikiwemo Baraza la Habari Tanzania (MCT) na wengine wawili walifungua kesi katika Mahakama ya Afrika Mashariki namba 2, 2017.

“Katika kesi hiyo Mahakama ya Afrika Mashariki ilitoa hukumu iliyoeleza kuwa sheria hiyo inakiuka haki za msingi na kuvitaja baadhi ya vifungu.

“Baadhi ya vifungu vya 7, 21, 35, 36, 37, 38, 39, 40, 50, 51, 52, 53, 58 na 59 vya Sheria ya Huduma za Habari inakiuka Mkataba wa Afrika Mashariki na ili kuepuka vifungo lazima waandishi wa habari waandike habari zinazoipendelea serikali,”amesema Kambole.

Kambole ameongeza kuwa kupitia sheria hiyo vyombo vya habari haviko huru katika kutekeleza majukumu hivyo kupelekea kutokuwepo kwa habari za kiuchunguzi ambazo husaidia maendeleo ya Taifa ikiwemo masuala ya rushwa na mengine.

Hata hivyo Kambole amebainisha kuwa sheria hiyo pia inatoa mamlaka ya mwandishi wa habari kunyang’anywa utambulisho wake au kibali cha kufanya kazi za uandishi hivyo kutoa hofu kwa wahusika kutofanya kazi yao ili kulisaidia taifa.

Awali Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Nevile Meena  amesema Bodi ya Ithibati ya Habari ikiwa itaundwa na Serikali  basi itakosa uhuru wa kufanya uamuzi pale malalamiko yatakapoihusu yenyewe (serikali).

Meena ambaye ni Katibu Mstaafu wa TEF amesema, ili kukwepa hilo na kutenda haki kwa vyombo vyote vya habari nchini, hakuna budi kwa Bodi ya Ithibati ya Habari kuundwa na kusimamiwa na wanataaluma haswa wanahabari.

Next Post
Nape awatoa hofu wanahabari

Nape awatoa hofu wanahabari

Sabasaba

Sabasaba

TEF yaongeza  nguvu Mabadiliko ya Sheria

TEF yaongeza nguvu Mabadiliko ya Sheria

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In