• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

TEF yaongeza nguvu Mabadiliko ya Sheria

by bajeti
July 16, 2022
in Habari
0
TEF yaongeza  nguvu Mabadiliko ya Sheria
Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO

JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limeteuwa wahariri sita kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini kusaidia  mchakato wa mabadiliko ya sheria za habari nchini.

Wahariri hao ambao watakuwa na jukumu la kuwasimamia waandishi wa habari waandamizi  kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini ili kujikita katika kuelekea mabadiliko ya sheria ya habari.

Akizungumza wakati wa kikao cha kuteua Kikosi Kazi hicho katika Ofisi za TEF jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Deodatus Balile amesema wanapaswa kuwa na waandishi wabobezi katika harakati hizo, hali iliyopelekea  kuundwa kwa timu ya wanataaluma ambao watawasimamia waandishi ili waweze kupita njia itakayoleta mafanikio.

Amesema uteuzi huo unalenga  kuongeza chachu ya harakati kuelekea mabadiliko ya Sheria za habari nchini.

“Timu hii ya wataalamu wabobezi, itasaidia kwa kiwango kikubwa kunyoosha mwelekeo na hatimaye kupata matokeo chanya,” amesema Balile.

Wahariri hao walioteuliwa na TEF kuwasimamia waandishi (mentors) ni Joseph Kulangwa wa gazeti la  Raia Mwema, Stella Aron- Majira, Rashidi Kejo  -Mwananchi, Angela Mang’enya wa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC)  pamoja na Wahariri wastaafu Joseph Nakajumo na Midladjy Maez.

TEF imebainisha kuwa Angela Mang’enya amepangwa kuwakufunzi Fatma Hassan Ali (Channel Ten), Kissa Daniel (East Africa TV), Faridy Mohammed (Mlimani TV), Godfrey Monyo (ITV).

Aidha Joseph Nakajumo atawasimamia Christopher James (Radio One), Salma Juma (Classic Fm), Philip Nyiti (Clouds Media) na Brumo Bomola (Radio Tumaini).

Kwa upande wa Rashid Kejo atawaongoza  waandishi Regina Mkonde (Mwanahalisi Online), Faraja Masinde (Mtanzania Digital), Brighter David (Daily News Digital) na Iddy Lugendo wa Majira.

Joseph Kulangwa amepangiwa Alex Kazenga (Jamhuri Media), Peter Elias (Mwananchi), Mery Geofrey (Nipashe) na Goodluck Hongo wa Tanzania Daima.

Waandishi wengine ni Anneth Nyoni (Tumaini TV), Humphrey Msechu (Spatklight TV), Jackline Martin (Times Majira) na Yusuph Digossi (IBN TV) watakuwa chini ya Stella Aron

Kwa upande wa Maez atakuwa na kazi ya kupitia kazi na kuandika ripoti.

Next Post
Uzinduzi wa Maabara

Uzinduzi wa Maabara

Joto lauwa watu 500 Uhispania

Joto lauwa watu 500 Uhispania

Serikali kuajiri Maafisa Ugani zaidi ya 300

Serikali kuajiri Maafisa Ugani zaidi ya 300

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In