• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Serikali kuajiri Maafisa Ugani zaidi ya 300

by bajeti
July 22, 2022
in Habari
0
Serikali kuajiri Maafisa Ugani zaidi ya 300

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki akizungumza na wadau wa Sekta ya Mifugo na (hawapo pichani) uliofanyika jijini Dodoma Jana.(picha na mpigapicha wetu)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU, Dodoma

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amesema Serikali itaajiri Maafisa Ugani zaidi  ya 300 ili kupunguza changamoto ya uhaba wa wataalamu hao.

Mbali na hilo lakini pia watanunua  pikipiki zaidi ya 1000 kwa ajili ya kuwawezesha maafisa hao kutekeleza majukumu yao kwa urahisi.

Ndaki ametoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano wa wadau kutoka Sekta ya Mifugo uliofanyika jijini Dodoma jana.

Ndaki amesema kwa mwaka huu wa fedha serikali itatoa ajira hizo na kununua pikipiki hizo ili kuwasaidia kuwafikia kwa wakati wafugaji hasa wakati huu ambapo kutakuwa na kampeni kubwa ya kutoa elimu kwa wafugaji ili kufuga kisasa na kuchangia pato la Taifa.

Amesema wafugaji wengi nchini bado wanafuga kienyeji  na kupelekea sekta ya mifugo kutokuwa na tija kubwa, hivyo ni wakati sasa watafiti wasaidie kutatua changamoto hiyo.

“Kama tutaendelea kufuga kama tunavyofuga leo kwa kuswaga Ng’ombe, baada ya miaka 10 ijayo tutaleta shida kwenye nchi hii, kwa sababu maeneo ya malisho yamepungua, hivyo watafiti watusaidie kuja na majibu yanayolenga kutatua changamoto hii, tuone namna gani tutakabiliana na jambo hili”, amesema Ndaki

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wadau wa Sekta binafsi waliohudhuria Mkutano wa Wadau wa Mifugo uliofanyika jijini Dodoma Jana. Kulia kwake ni Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Dkt. Charles Mhina.

Aidha amebainisha kuwa  kwa mwaka huu wa fedha wao kama wizara   wamejipanga kufanya kampeni kubwa ya kuwaelimisha wafugaji nchi nzima kuhusu ufugaji bora na wenye tija.

“Tutaanza kutoa elimu  mwaka huu kuwaelimisha wafugaji kuhusu ufugaji bora na tutaendelea mpaka ujumbe huu wa kufuga kwa tija uwe umefika kwa wafugaji wote nchini”, ameeleza Ndaki

Aliendelea kusema kuwa Wizara imetenga bajeti kwa ajili ya kuelimisha wafugaji kuhusu malisho ya mifugo na mabadiliko ya tabia nchi ili wabadilike kutoka kufuga kiasili na kufanya ufugaji wa kibiashara.

Naye, Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Dkt. Charles Mhina amesema maendeleo ya Sekta ya Mifugo kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na sekta binafsi.

“ Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wadau hao ili sekta hiyo iweze kuwa na mchango mkubwa katika pato la taifa”amesema Dkt.Mhina

Next Post
Serikali:Wazazi saidieni kuwalinda watoto

Serikali:Wazazi saidieni kuwalinda watoto

Sheria mpya kuwabana watoa fedha kwa ombaomba

Sheria mpya kuwabana watoa fedha kwa ombaomba

DODOMA

DODOMA

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In