• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Serikali:Wazazi saidieni kuwalinda watoto

by bajeti
July 23, 2022
in Habari
0
Serikali:Wazazi saidieni kuwalinda watoto

Maofisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dar es Salaam wakimsikiliza Mratibu wa Mradi wa Kuimarisha Familia kutoka Sos Children’s Villages Kennedy Mshema (hayupo pichani) wakati wa uundaji wa mabaraza na madawati ya watoto shuleni uliofanyika jana jijini Dar es Salaam (Picha na mpigapicha wetu)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

MKURUGENZI Msaidizi wa Watoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Mathias Haule amesema wazazi wanajukumu kubwa la kuhakikisha usalama wa watoto unakuwepo.

Kauli ya Haule imekuja wakati ambao ongezeko la vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vikiongezeka kwa kasi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati wa kuanza kwa uundaji wa mabaraza na madawati ya watoto shuleni  kwa kuwahusisha maofisa Ustawi wa Jamii kutoka Mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na Sos Children’s Villages,Haule amesema  jukumu la kulinda usalama na kupinga ukatili dhidi ya watoto ni kila mzazi

Mkutano huo ambao umewashirikisha wadau na mashirika ya kupinga ukatili dhidi ya watoto umekuja siku chache baada ya kuzinduliwa kwa Mwongozo mpya wa Taifa wa Uundaji na Uendeshaji wa Mabaraza ya Watoto Tanzania jijini Dodoma.

Alisema Serikali inaendelea kupokea maoni ya wadau na kuyafanyia kazi katika kuhakikisha kuwa watoto wanalindwa dhidi ya ukatili.

Alisema wao kama Wizara wamewezesha kuanzishwa kwa madawati na mabaraza ya watoto lakini jukumu la kuimarisha ulinzi wa watoto ni la kila mtanzania.

Mratibu wa Mradi wa Kuimarisha Familia kutoka Sos Children’s Villages Kennedy Mshema akizungumza na Maofisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa uundaji wa mabaraza na madawati ya watoto shuleni uliofanyika jana jijini Dar es Salaam (Picha na mpigapicha wetu)

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa Kuimarisha Familia kutoka Sos Children’s Villages Kennedy Mshema  alisema wao wamekuwa na miradi mbalimbali ikiwemo kuwakutanisha wadau ili kuhakikisha kuwa ushiriki wa watoto katika kutambua haki zao pamoja na ulinzi ili kuondoa ukatili dhidi yao.

“Sisi SoS Children’s Villages kwa kushirikiana na Serikali kupitia Mkoa wa Dar es Salaam tumeanza uundwaji wa mabaraza ya watoto na madawati  ya watoto shuleni.

“Tumewezesha wanafunzi kushiriki kikamilifu siku ya Mtoto wa Afrika ikiwemo kuzishirikisha shule za Zingiziwa na Chakina kama shule za mfano katika juhudi za kupinga ukatili dhidi ya watoto”alisema Mashema.

Kwa upande wake Mwanafunzi wa darasa la saba kutoka Shule ya Msingi Mjimwema iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam Jovitha Joel alisema katika mkutano huo yeye kama mwanafunzi amejifunza mambo mengi ikiwemo kujua ukatili dhidi ya watoto.

“Nilikuwa sijui lakini sasa najua ukatili ni nini na nitaenda kutoa elimu hii kwa wanafunzi wenzangu na jamii inayonizunguka”alisema Joel

Next Post
Sheria mpya kuwabana watoa fedha kwa ombaomba

Sheria mpya kuwabana watoa fedha kwa ombaomba

DODOMA

DODOMA

Serikali yatenga vyumba 100 kuhudumia  watoto njiti

Serikali yatenga vyumba 100 kuhudumia watoto njiti

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In