• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, May 5, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Serikali yatenga vyumba 100 kuhudumia watoto njiti

by bajeti
July 26, 2022
in Habari
0
Serikali yatenga vyumba 100 kuhudumia  watoto njiti

Makamu wa Rais wa Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation inayojihusisha na kusaidia Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti). Doris Mollel, mara baada ya Mazungumzo yaliofanyika Jijini Dar es salaam jana.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amesema Serikali imetenga Sh.Bilioni 23.36  ya Wizara ya afya kwa mwaka 2022/23 na kutenga vyumba 100 vitakavyosaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti) ili kupunguza vifo  vyao.

Dkt.Mpango ameyasema hayo jana Julai 25,2022 jijini Dar es Salaam baada ya kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation inayojihusisha na kusaidia Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti) Doris Mollel.

Amesema serikali imeendelea kusogeza huduma za afya karibu na wananchi kwa ujenzi wa hospitali za wilaya, vituo vya afya katika kata pamoja na zahanati katika vijiji ili kuendelea kukabiliana na changamoto za vifo vya mama na mtoto.

Dkt.Mpango ametoa wito kwa wadau, taasisi za dini pamoja na wananchi kwa ujumla kulipa kipaumbele suala la kuwasaidia Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati ili kukabiliana na changamoto ya vifo vinavyotokana na hali hiyo.

Aidha Dkt.Mpango ameongeza kuwa ni muhimu pia kwa taasisi inapaswa kuwekeza pia katika utoaji elimu ya afya ya uzazi ili kukabiliana na ongezeko la Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati kwani maeneo mengi hasa ya vijijini wanashindwa kupata uelewa juu jambo hilo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Philip Mpango akizungumza  na Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation inayojihusisha na kusaidia Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti) Doris William Mollel jijini Dar es Salaam jana (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation  Doris Mollel amempongeza Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango  kwa jitihada alizofanya za kutambua changamoto zinazojitokeza katika malezi ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati  na kuchangia vifaa tiba katika Hospitali ya Taifa Muhimbili hivi karibuni.

Aidha ameishukuru serikali kwa kuendelea kuiunga mkono taasisi hiyo husasani katika ajenda ya mtoto njiti na tayari wamewasilisha ombi la kuongezwa likizo kwa wanaojifungua kabla ya wakati ikiwemo kuwekwa elimu ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati katika masomo ya sayansi kwa shule za msingi na baiolojia kwa shule za sekondari.

 

 

Next Post
Majaliwa: Tutasimamia madai ya madereva na haki za waajiri

Majaliwa: Tutasimamia madai ya madereva na haki za waajiri

Wananchi watakiwa kuitunza miradi ya  EBARR

Wananchi watakiwa kuitunza miradi ya EBARR

Mawaziri nchi  18  zinazozalisha almasi wakutana  Arusha

Mawaziri nchi 18 zinazozalisha almasi wakutana Arusha

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:8
  • Today's page views 8
  • Total visitors 16,072
  • Total page views 18,232

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In