• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Wananchi watakiwa kuitunza miradi ya EBARR

by bajeti
July 27, 2022
in Mazingira
0
Wananchi watakiwa kuitunza miradi ya  EBARR

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Switbert Mkama (mwenye miwani) akiangalia bidhaa za ngozi katika kiwanda cha ngozi ambacho ni sehemu ya Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) katika Kijiji cha Jitegemee wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati wa ziara yake mkoani humo leo(Picha na Mpigapicha wetu)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,MANYARA

SERIKALI imewataka wanufaika wa mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) kuutunza ili iwanufaishe.

Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira  Dkt. Dkt. Switbert Mkama  wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua shughuli mbalimbali za mradi huo zinazofanyika katika vijiji vya Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara.

Akizungumza na wanachama wa kiwanda kidogo cha kutengeneza bidhaa za ngozi katika Kijiji cha Jitegemee, Dkt. Mkama mbali ya kuwapongeza kwa kuendeleza ushirikiano katika kuendesha shughuli zao.

“Tumeridhika na maendeleo yenu, huu mradi ni wa kwenu sio wa Serikali kwa hiyo nawaomba muutunze mradi huu kwa ajili yenu na pia uwe darasa kwa wengine ili nao waige mfano wenu, kwani ninyi mkifanya vizuri na wengine wataiga na hivyo mtakuza uchumi wa wananchi wa hapa,” alisema Dkt. Mkama.

Aidha, Dkt.,Mkama aliwashauri kuhifadhi benki na kutumia vizuri fedha zinazotokana na mauzo ya bidhaa zao za ngozi wanazozalisha ili ziwasaidie kupata maendeleo.

Hata hivyo Dkt. Mkama aliahidi Serikali baadhi ya changamoto zinazowakabili ikiwemo kuwapelekea vitendea kazi.

Dkt.Mkama alimuelekeza pia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro kusimamia zoezi hilo.

Wakizungumza mbele ya kiongozi huyo baadhi ya wananchi wanufaika wa Mradi wa EBARR waliishukuru na kuipongeza Serikali kwa kuwajali katika changamoto ya mabadiliko ya tabianchi inayowakabili.

 

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Switbert Mkama (wa kwanza mbele) akikagua shughuli ya josho la mifugo katika Kijiji cha Irkujit ambayo ni sehemu ya Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais katika Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara(Picha na mpigapicha wetu).

Mwenyekiti wa kikundi kinachojihusisha na uzalishaji wa bidhaa za ngozi Zaina Shekilango alimshukuru Naibu Katibu Mkuu lakini pia aliomba viongozi waendelee kuvitembelea vikundi vyao ili waendelee kupata elimu kuhusu namna bora ya kusimamia mradi wao kwani bado wanaendelea kujifunza.

Mbali na kiwanda hicho kidogo pia katika ziara hiyo Dkt. Mkama alitembelea na kukagua shughuli mbalimbali zikiwemo josho la mifugo na birika la kunyweshea mifugo, uchimbaji wa lambo jipya pamoja na ufugaji wa mbuzi 50 katika Kijiji cha Irkujit.

Maeneo mengine aliyotembelea ni mabanda mawili ya kuku wa mfano na kuku 850 kwa vikundi vya ufugaji wa kuku katika vijiji vya Jitegemee na Mkumbi.

Dkt. Mkama yupo katika ziara ya kutembelea na kukagua shughuli zinazotekelezwa kupitia Mradi wa EBARR chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais katika wilaya mbalimbali.

 

 

Next Post
Mawaziri nchi  18  zinazozalisha almasi wakutana  Arusha

Mawaziri nchi 18 zinazozalisha almasi wakutana Arusha

Serikali kuzindua My Dustbin

Serikali kuzindua My Dustbin

Majaliwa :Tunatambua mchango wa wanawake katika ukuaji wa uchumi

Majaliwa :Tunatambua mchango wa wanawake katika ukuaji wa uchumi

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In