• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Serikali kuzindua My Dustbin

by bajeti
July 30, 2022
in Mazingira
0
Serikali kuzindua My Dustbin

Waziri wa Nchi Osi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Selemani Jafo (aliyebeba mzigo) akibeba taka na kuzipeleka katika vyombo maalumu vya kuhifadhi mara baada ya kushiriki katika zoezi la usafi wa mwisho wa mwezi katika Soko la Bonanza jijini Dodoma leo.(Picha na mpigapicha wetu)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,DODOMA

 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira  Selemani Jafo amesema Serikali inatarajia kuzindua kampeni ya usafi wa mazingira itakayofahamika kama My Dustbin kwenye mitaa mbalimbali nchi nzima.

Waziri Jafo ametoa kauli hiyo leo Julai 30,2022 jijini Dodoma wakati akizungumza na wafanyabiashara  katika zoezi la usafi wa mwisho wa mwezi katika Soko la Bonanza.

Amesema kampeni hiyo itasaidia kuweka mitaa katika hali ya usafi kwa kuwa kila mwananchi anatakiwa kutupa taka kwenye mapipa yaliyopo kwenye mitaa badala ya kutupa hovyo kwani agenda ya mazingira ni endelevu na kila mtu anapaswa kuitekeleza kwavitendo

“Ndugu zangu agenda ya mazingira ni endelevu sote yatupasa kuitekeleza kwa vitendo na uwe ni utamaduni wetu sote”amesema Jafo

Hata hivyo,Waziri Jafo amewapongeza wafanyabiashara katika soko hilo kwa kuwa  mabalozi wa mazingira na wananchi kwa ujumla kwa kujitokeza kushiriki kufanya usafi wa mazingira

Wakati huo huo Jafo amemwelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) ndani ya kipindi cha siku 14 kuhakikisha anafanya ukarabati wa mfumo wa maji taka katika soko hilo ili kuondoa adha inayowakumba wafanyabiashara kwa sasa.

“Ukarabati huu wa Mfumo wa maji taka katika eneo hili ufanyike mara moja, Mkurugenzi wa DUWASA asimamie kwa karibu utekelezaji wake” amesisitiza Jafo.

Waziri wa Nchi osi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Selemani Jafo akizungumza na wafanyabiashara katika Soko la
Bonanza jijini Dodoma mara baada ya kushiriki zoezi la usa
katika soko hilo leo(Picha na mpigapicha wetu)

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu wa Jiji la Dodoma Dickson Kimaro amesema wamekuwa wakihamasisha wananchi kushiriki usafi wa mazingira ili kuweka jiji katika hali ya usafi.

Aidha Kimaro amesitiza uwajibikaji wa kila mwananchi katika kuhakikisha usafi unafanyika mita tano kuzunguka maeneo ya makazi na biashara.

Ameongeza kuwa katika soko hilo wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla wamekuwa wakijitokeza kushiriki katika kufanya usafi wa mazingira sokoni hapo hivyo kuliweka jiji katika hali ya usafi.

 

 

 

Next Post
Majaliwa :Tunatambua mchango wa wanawake katika ukuaji wa uchumi

Majaliwa :Tunatambua mchango wa wanawake katika ukuaji wa uchumi

Kigoma

Kigoma

SONGWE

SONGWE

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:8
  • Today's page views 8
  • Total visitors 13,064
  • Total page views 14,809

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In