NA MWANDISHI WETU
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inatambua mchango mkubwa unaotolewa na wahandisi wanawake wanazozifanya katika kuchangia ukuaji wa uchumi nchini.
Amesema Serikali inatambua umuhimu wa tasnia ya uhandisi kwa ustawi wa nchi nzima, hivyo inahitaji kuhamasishwa na kupewa kipaumbele ikiwa ni pamoja na kutengeneza viongozi wengi zaidi wanawake katika tasnia ya uhandisi.
Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo jana (Ijumaa Julai 29, 2022) jijini Dar es Salaam wakati akizindua Kongamano la Saba la Wahandisi Wanawake.
Amesema amefurahishwa na shughuli za taasisi zinazofanywa na taasisi hiyo zimekuwa msaada mkubwa kwa Serikali katika kufanikisha azma yake ya kuwafikia Watanzania wote kuhusu kupata elimu ya masuala ya kihandisi.
“Mheshimiwa Rais amekuwa kielelezo cha ubora, maono, uthabiti na uthubutu kwa viongozi wanawake.
“Kupitia uongozi wake tumeshuhudia namna anavyoifungua nchi yetu ikiwa ni pamoja na kufungua njia kwa wanawake wengi kuwa na uthubutu na kujiamini .Sasa njia iko wazi kwenu, kazaneni na wekeni bidii ili kazi yenu iendelee kuonekana na Taifa lisonge mbele.”
Ameongeza kuwa Serikali imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuhamasisha wasichana katika shule za sekondari wapende na kusoma masomo ya sayansi na hisabati.
“Serikali inatambua mchango wa taaluma ya uhandisi kwa fani mbalimbali katika ukuaji wa uchumi wa Taifa kupitia ufanikishaji na ukuaji wa huduma mbalimbali.”amesisitiza Waziri Mkuu Majaliwa




Discussion about this post