NA MWANDISHI WETU,ARUSHA
BARAZA la Mawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Afrika zinazozalisha Almasi wanakutana jijini Arusha katika mkutano wa tatu wa dharura likiwa na lengo la kuidhinisha nyaraka muhimu za Jumuiya hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha jana,Waziri wa Madini Dotto Biteko amesema kuwa mkutano huo imejumuisha nchi 18 zikiwemo 12 za wanachama zinazozalisha almasi na sita za waangalizi ambazo jiolojia yake inauwezo wa kuzalisha madini na kuwa wazalishaji wa almasi siku za usoni.
Biteko amesema ni heshima kubwa kama nchi kuwajibika kwa ajili ya maendeleo ya nchi hususani katika usimamizi wa madini ya almasi ambapo wameweza kupitia upya kwa mifumo ya Jumuiya hiyo ikiwemo marekebisho ya Katiba,Kanuni na miongozo mbalimbali ya Jumuiya.
Aidha ameongeza kuwa kama nchi wameweza kujifunza zaidi kuhusu usimamizi wa sekta hususani kwa madini ya almasi ambapo pia nchi wanachama na hata wasio wanachama walipata nafasi ya kuja kujifunza kuhusu namna nchini ilivyofanikiwa kuwaendeleza wachimbaji wadogo wakiwemo wa madini ya almasi na dhahabu.
“Lakini pia namna ambavyo serikali ilivyoweza kusimamia mifumo inayohusisha mnyororo mzima wa shughuli za madini.”aliongeza Biteko
Aidha Biteko amebainisha kuwa katika mkutano wa pili wa kawaida wa baraza hilo uliofanyika Aprili 7 na 8 mwaka huu nchini Zimbabwe ,Tanzania kama Mwenyekiti waliongoza mkutano huo ambapo Kamati ya wataalam walichambua na kujadili nyaraka mbalimbali zinazohusiana na mapitio na marekebisho ya nyaraka zinazosimamia jumuiya hiyo.
Aidha Biteko amebainisha kuwa Jumuiya ya Wazalishaji wa Almasi ilianzishwa kwa mujibu wa Azimio la Rwanda na Angola mwaka 2006 kwa lengo la kuunda Baraza la Mawaziri wa jumuiya hiyo ni kupata nchi zinazozalisha almasi Afrika na Jukwaa la kuzikutanisha nchi zote za Afrika katika kusudi moja la kuhakikisha rasilimali za madini hayo zinanufaisha nchi wanachama.




Discussion about this post