• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Monday, May 25, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Joto lauwa watu 500 Uhispania

by bajeti
July 21, 2022
in Mazingira
0
Joto lauwa watu 500 Uhispania

Moto ukiunguza misitu nchini Ugiriki kutokana na kuongezeka kwa joto kali hali iliyopoelekea mamia ya watu kuuawa(picha kwa hisani ya mtandao)

Share on FacebookShare on Twitter

MADRID UHISPANIA,

WAZIRI Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez amesema zaidi ya watu 500 wamepoteza maisha nchini humo wakati wa wimbi la joto la siku 10 huku bara lote la Ulaya likiendelea kupata hasara kubwa kutokana na joto kali ambalo limevunja rekodi mwaka huu.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Pars.limemnukuu Sanchez jana akisema kuwa  hali hivi sasa ni ya hatari na kuongeza kuwa mabadiliko ya tabianchi ni ukweli ambao hauwezi kupingika huku akiwahimiza wananchi kuchukua tahadhari.

Sanchez amesema takwimu hizo za waliopoteza maisha zimewasilishwa na Taasisi ya Afya ya Carlos III ambayo inakadiria idadi ya vifo vinavyotokana na joto itaongezeka mwaka huu ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Nyuzijoto katika baadhi ya maeneo ya Uhispania ni zaidi ya 45 na joto hilo limepelekea misitu kuteketea moto.

Nchini Uingereza  joto pia limeongezeka mwaka huu na kuvunja rekodi  ambapo mashariki mwa Uingereza kumeripotiwa nyuzi joto  40.3C na hivyo kupita kiwango cha juu cha hapo awali mnamo 2019.

Kaskazini mwa Ureno, rubani alifariki wakati ndege yake ya kusaidia shughuli za zima moto ilipoanguka katika eneo la Foz Coa, karibu na mpaka wa Uhispania.

Mamlaka ya Ureno inasema takriban watu 238 wamekufa kutokana na joto hilo kali katika wiki iliyopita.

Kwa sasa joto duniani limeongezeka kwa takriban nyuzi joto 1.1C tangu enzi ya viwanda ianze na halijoto itaendelea kuongezeka kama serikali kote ulimwenguni hazitafanya juhudi za kupunguza kiwango cha uzalishaji wa kaboni.

Next Post
Serikali kuajiri Maafisa Ugani zaidi ya 300

Serikali kuajiri Maafisa Ugani zaidi ya 300

Serikali:Wazazi saidieni kuwalinda watoto

Serikali:Wazazi saidieni kuwalinda watoto

Sheria mpya kuwabana watoa fedha kwa ombaomba

Sheria mpya kuwabana watoa fedha kwa ombaomba

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:0
  • Today's page views 0
  • Total visitors 16,454
  • Total page views 18,665

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In