• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Serikali kuwachukulia hatua waingizaji vifaranga kwa magendo

by bajeti
July 12, 2022
in Habari
0
Serikali kuwachukulia hatua waingizaji vifaranga kwa magendo

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (wa kwanza kushoto) akipatiwa maelezo na mtaalamu wa mitambo ya kuzalisha vifaranga(jina halikupatikana)kuhusu kifaa kinachoonesha ukuaji wa kifaranga ndani ya yai wakati alipotembelea Shamba la Ogania linalotumika kuzalisha vifaranga vya kuku lililopo wilayani Kibaha, Mkoa wa Pwani jana.(Picha na mpigapicha wetu)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,PWANI

SERIKALI haitavumilia vitendo vya uingizwaji wa vifaranga vya kuku kwa njia za panya hapa nchini kwa sababu vinasababisha nchi kukosa mapato ikiwemo kurudisha nyuma jitihada za uwekezaji nchini.

Onyo hilo limetolewa Julai 11,2022 na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega wakati wa ziara yake wilayani Kibaha, mkoani Pwani alipotembelea mashamba ya kutotoleshea vifaranga vya kuku ya Organia na Mkuza Chicks.

Akizungumza na wawekezaji wa mashamba hayo kwa nyakati tofauti, Waziri Ulega amesema kuanzia sasa wataalamu waliopo wilayani na katika mipaka yote ya nchi watakuwa makini kufuatilia kwa karibu na wale wote wanaoingiza vifaranga kiholela na wakabainika watawajibishwa.

“Hawa watu wanaoingiza vifaranga kienyeji bila kufuata sheria, taratibu na kanuni zetu sio tu wanasababisha nchi kukosa mapatoa bali wanaangusha uwekezaji wa ndani ya nchi na uchumi kwa ujumla”, amesema Ulega

Amesema ni muhimu kwa wataalamu wanaohusika na usimamizi wa vibali vya kuingiza vifaranga kuandaa mfumo madhubuti utakaokuwa na taarifa zitakazowezesha serikali kujua na kusimamia vizuri zoezi hilo la utoaji vibali.
“Tunamshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan amefanya kazi nzuri sana ya kualika wawekezaji nchini, sasa ni kazi yetu kila mmoja kulinda uwekezaji wa namna hii”amebainisha Ulega

Aidha, alitumia fursa hiyo pia kuwaomba Wafugaji wa kuku nchini kuziamini kampuni zinazozalisha vifaranga hapa nchini huku akiongeza kuwa kama kuna changamoto yoyote inayotokana na wazalisha hao basi wasisite kuziwasilisha wizarani ili zifanyiwe kazi kwa lengo la kuboresha huduma hiyo.

“Lakini vilevile tunaponunua vifaranga vya hapa nyumbani inasaidia kukuza uchumi wetu, kuweka usalama wa uwekezaji tunaowaalika kuja kuwekeza hapa nchini,” ameongeza Ulega

Awali, wawekezaji wa Mkuza Chicks na Organia walieleza kuwa changamoto kubwa wanayokabiliana nayo kwa sasa ni uingizwaji holela wa vifaranga kutoka nje jambo ambalo linasababisha biashara hiyo kutokuwa ya uhakika.

Next Post
Watafiti sekta ya uvuvi watakiwa kuibua fursa

Watafiti sekta ya uvuvi watakiwa kuibua fursa

Kambole:Makosa tasnia ya habari yasiwe kosa la jinai

Kambole:Makosa tasnia ya habari yasiwe kosa la jinai

Nape awatoa hofu wanahabari

Nape awatoa hofu wanahabari

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In