• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Majaliwa:Viongozi fuateni falsafa ya Serikali kuhudumia wananchi

by bajeti
August 2, 2022
in Habari
0
Majaliwa:Viongozi fuateni falsafa ya Serikali kuhudumia wananchi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka washiriki wa kozi fupi ya 13 ya viongozi katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi kusimamia falsafa ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan iliyojielekeza katika kuwahudumia watanzania.

Majaliwa amesema lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwaongezea uelewa kuhusu masuala ya ulinzi na stratejia kwa ajili ya kulinda maslahi mapana ya Taifa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua kozi fupi ya 13 ya viongozi katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi.

Waziri Mkuu Majaliwa amefafanuwa kuwa  Serikali inatarajia kuona mabadiliko ya kimtazamo, ushauri na maamuzi watakayoyafanya kuakisi walichokipata kupitia kozi hiyo mara baada ya viongozi hao kurudi kwenye maeneo yao ya utendaji.

Amesema kozi hiyo pia itawaongezea uelewa na ufanisi katika eneo zima la ulinzi na stratejia kwa ajili ya kulinda maslahi mapana ya Taifa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Majaliwa  amebainisha kuwa Serikali inatarajia kwamba washiriki wote, watatumia kikamilifu fursa hiyo adhimu kushiriki kwa umakini na uhodari wa hali ya juu ili kuongeza uelewa wao wa masuala mtambuka hususani ya kiulinzi, kiusalama na kistratejia.

Kozi hiyo inahudhuriwa na baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Maafisa Waandamizi kutoka Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Taasisi za Kimkakati za Serikali.

Next Post
Dkt.Chana:Maliasili  yatengewa bajeti zaidi ya Sh.Bilioni 600

Dkt.Chana:Maliasili yatengewa bajeti zaidi ya Sh.Bilioni 600

Mkandarasi apewa siku 14 kukamilisha mradi EBARR

Mkandarasi apewa siku 14 kukamilisha mradi EBARR

Ziara Kilimanjaro

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:6
  • Today's page views 6
  • Total visitors 13,062
  • Total page views 14,807

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In