• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Mkandarasi apewa siku 14 kukamilisha mradi EBARR

by bajeti
August 3, 2022
in Mazingira
0
Mkandarasi apewa siku 14 kukamilisha mradi EBARR

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Switbert Mkama(mwenye miwani katikati)akipata maelezo kutoka kwa Erasto Nyahila (kushoto) ambaye ni mwakilishi wa Kampuni ya Babenko inayohusika na uchimbaji wa visima na ujenzi wa mnara wa tanki la maji katika Kijiji cha Mingo, Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro kupitia Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia mifumo Ikolojia Vijiijini (EBARR) unaosimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Switbert Mkama ametoa muda wa siku 14 kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Dabenko Enterprises Ltd kukamilisha ujenzi wa tanki la maji litakalotumika kutoa huduma ya maji kwa wakazi zaidi ya 1250 katika Kijiji cha Mingo, Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.

Dkt. Mkama ametoa agizo hilo leo Agosti 2, 2022 akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia mifumo ya Ikolojia Vijiijini  (EBARR) unaotekelezwa wilayani Mvomero.

Dkt. Mkama amemtaka Mkandarasi huyo kukamilisha haraka na kwa viwango vinavyokubalika ujenzi wa mnara wa tanki la maji na kurekebisha kasoro zilizoonekana.

“Hakikisha ujenzi huu unakamilka kama ilivyoelekezwa kwa mujibu wa mkataba na maboresho yafanyike katika maeneo ya umaliziaji na dirisha hili litolewe, liwekwe lenye viwango” amesisitiza Dkt. Mkama.

Hata hivyo Dkt.Mkama amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero kusimamia miradi hiyo ili thamani ya fedha ilingane na ubora wa kazi za mradi wenyewe.

Nae Mwakilishi wa Kampuni ya Dabenko inayohusika na ujenzi wa tanki hilo  Erasto Nyahila ameahidi kurekebisha kasoro zote zilizobainika ndani ya muda uliopangwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Mingo Rashid Athumani amesema kukamilika kwa uchimbaji na ujenzi wa kisima chenye urefu mita 150 katika Kijiji chao utasaidia shughuli za kilimo cha umwagiliaji mwaka mzima na matumizi ya nyumbani.

Sh.Bilioni 1.16 zimepelekwa katika wilayani humo kwa ajili ya ujenzi wa skimu ya umwagiliaji, uchimbaji wa visima vinne, malambo mawili, majosho mawili na kiwanda kidogo cha kuzalisha sabuni, kiwanda kidogo cha bidhaa za Ngozi, na kituo cha kukusanyia maziwa.

Shughuli nyingine zinazotekelezwa na Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikojia vijiijini kwa Wilaya ya Mvomero ni pamoja na ujenzi wa vitalu nyumba kwa ajili ya kilimo cha mbogamboga na majiko banifu kwa kaya 516.

Next Post

Ziara Kilimanjaro

Walionusurika bomu la nyuklia waandamana wakitaka yatokomezwe

Walionusurika bomu la nyuklia waandamana wakitaka yatokomezwe

Wafugaji waomba Maafisa Ugani kuwatembelea

Wafugaji waomba Maafisa Ugani kuwatembelea

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In