• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Wafugaji waomba Maafisa Ugani kuwatembelea

by bajeti
August 5, 2022
in Mazingira
0
Wafugaji waomba Maafisa Ugani kuwatembelea

Afisa Mifugo Mkuu kutoka Idara ya Uendelezaji wa Maeneo ya Malisho na Rasilimali za Vyakula vya Mifugo, Israel Kilonzo (kushoto) akitoa elimu kwa wafugaji wa Kanda ya Kaskazini kuhusu umuhimu wa kustawisha malisho ya mifugo alipokutana na wafugaji hao waliotembelea Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi lililopo kwenye maonesho ya Wakulima NaneNane Kanda ya Kaskazini yanayoendelea mkoani Arusha Agosti 4, 2022.(Picha na mpigapicha wetu)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MBARAKA KAMBONA, ARUSHA

WAFUGAJI wanaofanya shughuli zao Kanda ya Kaskazini wameiomba Serikali kuhakikisha Maafisa Ugani wanawafikia  ili kuwapatia huduma stahiki ili ufugaji wao uwe bora na wenye tija.

Wakizungunmza kwa nyakati tofauti katika Maonesho ya Wakulima NaneNane Kanda ya Kaskazini yanayofanyika mkoani Arusha leo, Wafugaji hao walisema ni muhimu maafisa ugani kuwatembelea wafugaji kila wakati na kutatua changamoto zinazowakabili.

Mmoja wa wafugaji hao Desderi Kimario amesema wanahitaji maafisa ugani wa Kilimo na Mifugo wote kwa pamoja wawe wanafanya kazi karibu na wafugaji ili wafugaji hao waweze kufanya shughuli zao kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu hao na kufanya ufugaji wao uwe na tija na nchi kwa ujumla.

“Tunaomba maafisa ugani wawe wanatutembelea mara kwa mara sisi wafugaji wadogo wadogo katika maeneo yetu huku kwenye Kata na Vijijini ili kujua matatizo yetu na sio mpaka tufike kwenye maonesho kama hivi, kwa sababu maonesho huwa ni mara moja kwa kila mwaka”, amesema Kimario Nayen Lawrence Kimambi, mfugaji kutoka mkoani Kilimanjaro amesema  kwa sasa ardhi imekuwa finyu hivyo ni muhimu wafugaji wakaendelea kupatiwa elimu ya kulima malisho ya mifugo ili kuokoa changamoto ya malisho na kuleta manufaa zaidi kwa jamii za wafugaji na nchi kwa ujumla.

Kwa upande wake Kevin Manase kutoka Arusha amesema kuwa kama wafugaji wataendelea kuelimishwa vizuri kuhusu umuhimu wa ulimaji wa malisho ya mifugo basi sio muda mrefu migogoro kati ya wakulima na wafugaji itakwisha.

Kwa Upande wake, Afisa Mifugo Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo, Israel Kilonzo aliwashauri wafugaji hao kuanza kujifunza namna ya  kustawisha malisho ya mifugo na kuachana na tabia ya kutegemea malisho ya asili peke yake  kwani kufanya hivyo kutasaidia kupunguza migogoro ya ardhi.

“Kama tunavyojua watu wanaongezeka na mifugo pia inaongezeka na ardhi iliyopo haitoshi kufanya ufugaji wa kuhamahama, ni lazima tujifunze kustawisha malisho  katika maeneo yetu na tujifunze kuyatumia vizuri ikiwemo kuwa na mifugo tutakayoimudu kuihudumia”, amesema Kilonzo

Next Post
SOS Children’s Villages yasaidia vikundi zaidi ya 30 kupambana ukatili dhidi ya mtoto

SOS Children’s Villages yasaidia vikundi zaidi ya 30 kupambana ukatili dhidi ya mtoto

Umri wa kuishi waafrika waongezeka miaka 10

Umri wa kuishi waafrika waongezeka miaka 10

Japan yaadhimisha miaka 77 ya kushambuliwa na bomu la atomiki

Japan yaadhimisha miaka 77 ya kushambuliwa na bomu la atomiki

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:6
  • Today's page views 6
  • Total visitors 13,062
  • Total page views 14,807

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In