NEW YORK,MAREKANI
MANUSURA wa bomu la atomiki lililodondoshwa mjini Hiroshima nchini Japan mwaka 1945 waliandamana jana jijini New York Marekani wakitaka silaha hizo kutokomezwa.
Maandamano hayo yamefanyika wakati wa mkutano wa mapitio ya Mkataba wa Kuzuia Ueneaji wa Silaha za Nyuklia unaoendelea jijini humo.
Watu wapatao 100 walishiriki maandamano hayo nje ya jengo la Umoja wa Mataifa ambapo maandamano hayo yalipangwa na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali.
Sakuma Kunihiko ambaye ni manusura aliyeshuhudia mji wa Hiroshima ukishambuliwa kwa bomu hilo alishiriki maandamano hayo huku akiwa amebeba bango lililosema kwamba ubinadamu na dunia zinakuja kwanza.




Discussion about this post