• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Sunday, January 18, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Aweso awataka wakuu mabonde ya maji kulinda vyanzo vya rasilimali hiyo

by bajeti
August 26, 2022
in Mazingira
0
Aweso awataka wakuu mabonde ya maji  kulinda vyanzo vya rasilimali hiyo

Waziri wa Maji Jumaa Aweso

Share on FacebookShare on Twitter

NA MIRIAM SARAKIKYA,ARUSHA.

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amewataka wakuu wa mabonde ya maji nchini kulinda vyanzo vyao vya rasilimali hiyo ikiwemo kuweka mipaka ili visivamiwe na wananchi.

Aweso ameyasema hayo leo Agosti 26,2022 wilayani Arumeru katika Jiji la Arusha wakati akizindua Mradi wa Kuondoa Mchanga katika Mto Nduruma ili urejee katika mkondo wake wa asili.

Amesema ni muhimu kwa wakuu hao wa mabonde kushirikisha  taasisi nyingine  katika kulinda na kutunza vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja na kuweka mipaka.

Aweso amefafanuwa kuwa kulinda na kuweka mipaka itasaidia zaidi kulinda vyanzo hivyo vya maji na sio kuathiri mazao ya wananchi  pindi wanapotumia vyanzo hivyo kwa shughuli za kibinadamu.

Hata hivyo Aweso amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuongeza Sh.Milioni 100 katika mradi huo ili kufanikisha kukamilika kwake.

Wakati huo huo Aweso amewaelekeza viongozi wa Bonde la Mto Pangani kutoa mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya maendeleo ya wananchi katika Halmashauri ya Meru.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango amewashukuru madiwani wa  Halmashauri ya Meru kwa kuridhia kutoa Sh.Milioni 1,000,000 kwa kila kata ambazo zilianza kuondoa mchanga katika mkondo wa maji wa Mto Nduruma nakupunguza changamoto za wananchi.

Aidha amewaomba  viongozi wa Bonde la Mto Pangani wanaotekeleza mradi huo kuweka mipaka katika  mito ukiwemo mto huo ili wananchi waweze kuelewa na kuacha kufanya shughuli za kibinadamu kandokando ya mito.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Mto Pangani Segule Segule ambaye anatekeleza mradi huo amewashukuru wananchi  pamoja na viongozi wa Serikali  ambao wanashirikiana katika kutunza vyanzo vya maji.

Diwani wa Kata ya Shambaraiburka  John Mollel amebainisha kuwa athari za  mto huo zimekuwa zikisababisha madhara makubwa kwa wananch ikiwemo  kupoteza maisha kutokana na mafuriko wakati wa Mvua.

Next Post
Masanja:Wahifadhi jengeni mahusiano mazuri na wananchi kurahisisha kazi zenu.

Masanja:Wahifadhi jengeni mahusiano mazuri na wananchi kurahisisha kazi zenu.

Mchimbaji ajipatia tanzanite ya bilioni 2.24  Mererani

Mchimbaji ajipatia tanzanite ya bilioni 2.24 Mererani

Dodoma

Dodoma

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:24
  • Today's page views 24
  • Total visitors 13,181
  • Total page views 14,927

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In