• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Mchimbaji ajipatia tanzanite ya bilioni 2.24 Mererani

by bajeti
August 27, 2022
in Mazingira
0
Mchimbaji ajipatia tanzanite ya bilioni 2.24  Mererani

Waziri wa Madini Dkt.Dotto Biteko akionesha mawe ya madini ya tanzanite yaliyopatikana katika Mgodi wa Mererani Wilaya ya Simanjiro Mkoa wa Manyara leo Agosti 27,2022 wakati wa hafla ya ununuzi wa madini hayo.(Picha na mpigapicha wetu)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MIRIAM SARAKIKYA,MANYARA

WAZIRI wa Madini Dkt.Dotto Biteko amesema Serikali imeongeza uchunguzi katika Migodi ya Mererani ili kudhibiti baadhi ya wachimbaji wanaokiuka sheria na taratibu za uuzaji wa madini.

Dkt.Biteko ameyasema hayo leo Agosti 27,2022 katika ununuzi  wa jiwe la Tanzanite lililopatikana katika Mgodi wa Mererani Wilaya ya Simanjiro Mkoa wa Manyara  ambapo  mchimbaji Anselin Kawishe amefanikiwa kupata madini yenye thamani ya Sh.Bilioni  2.24.

Amesema awali kulikuwa na maafisa usalama sita katika eneo hilo lakini kwa sasa serikali imewaondoa na kuwaajiri wengine nane kutoka kitengo cha maafisa usalama .

Aidha amebainisha kuwa mfumo wa maisha kwenye uchimbaji wa madini unaongozwa na mifumo miwili ambayo ni uaminifu na utendaji kazi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa wizara hiyo Adolf Ndunguru  amewataka wachimbaji wadogo wa madini kufuata sheria zote za uchimbaji ili kufikia lengo la serikali

Amesema kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/23 wizara hiyo inapaswa kukusanya kiasi cha Sh.Bilioni 862 kila mwezi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere ameongeza kuwa   tangu kuamishwa shughuli za madini katika mkoa huo kipato cha halmashauri kimeanza kuongezeka.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Hundi ya Sh. Bilioni 2.24 Anslem Kawishe ameishukuru Serikali katika kuhakikisha kuwa wachimbaji wadogo wanafuata utaratibu ambao umesaidia kulindwa kwa madini hayo

Amesema  amekuwa mchimbaji mdogo wa madini hayo kwa miaka 15 sasa na licha ya kupata fedha hizo ataendelea na kazi hiyo.

Next Post
Dodoma

Dodoma

Serikali yabainisha mikakati kukabiliana na wanyamapori waharibifu

Serikali yabainisha mikakati kukabiliana na wanyamapori waharibifu

Bilioni 13 kupunguza migogoro ya binadamu na wanyamapori

Bilioni 13 kupunguza migogoro ya binadamu na wanyamapori

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In