• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Bilioni 13 kupunguza migogoro ya binadamu na wanyamapori

by bajeti
November 28, 2022
in Mazingira
0
Bilioni 13 kupunguza migogoro ya binadamu na wanyamapori

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja akiwa na Wahifadhi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania( TANAPA) na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) mara baada ya ziara ya kikazi katika Chuo cha Mafunzo ya Maliasili kwa Jamii Likuyu Sekamaganga Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma leo Septemba 8,2022.(picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)

Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO

 

SERIKALI imepokea Sh.Bilioni 13.2 kutoka Shirika la Ujerumani la GIZ kwa ajili ya mradi wa kupunguza migogoro baina ya binadamu na wanyamapori.

Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 8,2022 na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mary Masanja wakati wa ziara ya kikazi katika Chuo cha Mafunzo ya Maliasili kwa Jamii Likuyu Sekamaganga Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.

Amesema fedha hizo zitatumika katika mradi wa miaka mitatu wenye lengo la kutoa ujuzi kwa jamii kuhusu namna ya kukabiliana na wanyama wakali na waharibifu ambapo jamii hizo zitasambaza ujuzi kwa jamii nyingine hasa kwenye maeneo ya pembezoni mwa hifadhi.  .

Aidha, ameongeza kuwa  mafunzo hayo pia yatatolewa kwa Askari Wanyamapori wa Vijiji(VGS) ili kuongeza nguvu ya kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu.

“Rais Samia Suluhu Hassan ametafuta fedha kiasi cha Sh.Bilioni 13.2 ambazo zitatumika katika kufanya utafiti wa maeneo yenye changamoto za wanyama wakali na waharibifu, kutoa elimu kwa jamii zinazoishi pembezoni mwa hifadhi kuhusu uhifadhi na kukabiliana na wanyama wakali na waharibifu” amesema Masanja

Masanja amefafanuwa kuwa endapo jamii zikipata uelewa wa namna ya kuhifadhi na kukabiliana na wanyama wakali na waharibifu hakutakuwa na chuki baina ya binadamu na shughuli za uhifadhi.

Naye, Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Maliasili kwa Jamii Likuyu Sekamaganga, Jane John amesema kuwa chuo hicho kinatoa mafunzo ya Askari wa Wanyamapori wa Vijiji (VGS), Askari wa Misitu wa Vijiji.

“Tunatoa mafunzo kwa askari wanaosimamia fukwe za jamii, kozi kwa viongozi na wajumbe wa Kamati za Maliasili za Vijiji, Astashahada ya Utalii na Waongoza Watalii ikiwemo na mafunzo ya kudhibiti wanyama wakali na waharibifu”amesema John.

 

 

Next Post
Tanzania,Norway kushirikiana usimamizi rasilimali za bahari

Tanzania,Norway kushirikiana usimamizi rasilimali za bahari

RWANDA

RWANDA

SHIVYAWATA wataka vyombo vya habari kuwazingatia walemavu

SHIVYAWATA wataka vyombo vya habari kuwazingatia walemavu

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In